CCM Kirumba Watoto wa mtaa wa Kisha Mapanda washindwa kuzipasua Mbao za Ilemela.... Adhabu ya mwalimu aliye mafunzoni yawaangukia wanyukwa bakora 3-1 (inauma) nako Shinyanga Wapigadebe wa Stendi wailamba barafu ya Azam mara moko. Simba auwa Katikati ya jiji la Mbeya, Yanga yatafuna mashamba ma-3 ya Miwa. Kwa kina yaliyojiri dimbani ungana na #SPORTSRIPOTI usiku huu saa Tatu kamili hadi saa nne ukiwa na @elikanamathias @jumaayoo
YANGA 3-1 MTIBWA
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
YANGA SC imezinduka baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi tatu ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United na kulazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu Simba SC umerejesha matumaini kwa mabingwa hao watetezi.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na winga Mzambia, Obrey Chirwa ambaye leo alichezeshwa kama mshambuliaji pacha wa Amissi Tambwe.
Chirwa aliyesajiliwa msimu huu kutoka FC Platinums ya Zimbabwe, alifunga bao hilo kwa shuti akiwa ndani ya boksi akimalizia mpira ulioparazwa kwa kichwa na beki Andrew Vincent ‘Dante’ baada ya krosi ya winga Simon Msuva.
Yanga ingeweza kumaliza kipindi cha kwanza inaongoza kwa mabao zaidi, iwapo ingetumia vyema nafasi zaidi ya tatu nzuri ilizotengeneza za kufunga.
Kipindi cha pili, kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm alianza na mabadiliko akimpumzisha Deus Kaseke na kumuingiza Geoffrey Mwashiuya.
Pamoja na mabadiliko hayo, Yanga walijikuta wakiwaruhusu Mtibwa Sugar kusawazisha bao kupitia kwa winga wa zamani wa Simba SC, Haroun Chanongo dakika ya 63 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Tinocco.
Yanga wakatulia na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Msuva kabla ya mshambuliaji aliyetokea benchi Donald Ngoma kufunga la tatu dakika ya 80 akimalizia kazi nzuri ya Mwashiuya.
Yanga ikalazimika kumalizia pungufu mchezo huo baada ya mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kugongana na Shaaban Nditi na kupasuka kwenye dakika ya 87.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi saba, inazidiwa pointi saba na mahasimu wao wa jadi, Simba SC walio kileleni ingawa wamecheza mechi moja zaidi.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’/Mbuyu Twite dk74, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa/Donald ngoma dk73 na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk46.
Mtibwa Sugar; Benedicto Tinocco, Rogers Gabriel, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Shaaban Nditi, Ally Makalani, Mohammed Issa, Rashid Mandawa, Ibrahim Rajab ‘Jeba’/Hussein Javu dk66 na Haruna Chanongo/Kelvin Friday dk75.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.