ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 13, 2016

Dk.KIGWANGALLA AOMBEWA DUA NA SHEIKH MKUU WA MABOHORA DUNIANI.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akipata picha pamoja baadhi ya vijana ambao walipata kufunga ndoa na wake zao ndoa ambazo zaidi ya 50 zimefungwa huku Shehe Mkuu huyo wa Mabohora Duniani pia alipata kuzibariki.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla,   Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.