ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 20, 2016

USTAHIMILIVU HUSHINDA KATIKA UKWELI.

Ustahimilivu hushinda katika ukweli. Mara nyingi tuutupapo moto huo wa Roho Mtakatifu ili kuupata ukweli huwa tunazusha migawanyiko na mafarakano.

Ni nini sasa linapswa kuwa jibu la mfuasi wa Kristo? Ni kubaki katika ukweli ambao tumefunuliwa na tunauamini. “Tupige mbio kwa saburi tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”. 

Nabii Yeremia anakuwa mfano mzuri kwetu kwa kuufunua ukweli na kustahimili katika ukweli huo kiasi kwamba anatupwa katika bwawa la matope ili aangamie lakini mwishoni wanatokea wa kumsaidia kwa maana Neno la Mungu linatuambia kwamba atakayevumilia hata mwisho huyo ataokoka.

Nukuu ya Padre Joseph Peter Mosha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.