Wiki moja kabla ya Ligi Kuu England kuanza huwa ni kawaida kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii, mchezo ambao huzikutanisha timu Bingwa wa Ligi Kuu na Bingwa wa Kombe la FA, August 7 2016 England katika uwanja wa Wembley Leicester City ambaye ni Bingwa wa EPL na Man United ambaye ni bingwa wa FA.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha Jose Mourinho aliyejiunga na Man United msimu huu sambamba na nyota Zlatan Ibrahimovic aliyetumia mechi hiyo kudhihirisha ubora wake wa kucheka na nyavu, katika mchezo huo Man United wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Man United ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 31 kupitia kwa Jesse Lingard ila Leicester City walisawazisha goli hilo dakika ya 52 kupitia kwa mshambuliaji wao aliyeng’ara msimu uliopita Jarmie Vardy lakini furaha ya Leicester City ilimalizwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 83 na kuipa Man United ubingwa wa Ngao ya Hisani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.