ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 17, 2016

RC PWANI ACHUKIZWA NA KUKEMEA VIJANA WANASHINDA VIJIWENI BILA YA KAZI NA KUWA NA TABIA YA KUVUTA BANGI

NA VICTOR MASANGU,  RUFIJI

IMEELEWA kuwa nguvu kazi kubwa ya taifa inapotea bure kutokana na baadhi ya vijana wengine nchini Tanzania kuwa wavivu na kutojishughulisha na  shughuli  za kuleta maendeleo na badala yake wanaamua kujiingiza katika makundi ya uharifu,uvutaji wa madawa ya kulevya, pamoja na  kupoteza muda mwingi kushinda kutwa nzima wakiwa wamekaa vijiweni bila kazi yoyote.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa programu  ya kambi ya vijana ya kuwafundisha masuala ya  kilimo na  maarifa ambayo ipo chini ya mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto rufiji (RUBADA) iliyofanyika  katika kijiji cha Mkongo.

Ndikilo amebainishwa kwamb serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli isingependa kuona vijana wa kitanzania  hawataki kutumia fursa zilizopo na kuamua kujiingiza katika vitendo ambavyo vipo kinyume kabisa na taratibu na sheria zilizowekwa ambapo wakati mwingine zinaweza kusababisha vurugu.

Naye mwakilishi wa shirika la chakula  duniani (FAO) nchini Tanzania Fred Kafeero  amesema kwamba kulingana na ripoti zinaonyesha asilimia 70 ya vijana katika  africa hawana ajira hivyo kunahitajika juhudi za makusudi za kuweza kuwasaidia katika kilimo cha mboga mboga,huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Chwayo akiwaomba vijana hao kutumia fursa ya kilimo kupitia mafunzo watakayoyapata.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ameutaka uongozi wa RUDABA kuhakikisha kwamba wanaepukana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa dhidi yao na badala yake waweke mikakati endelevu ya kuwasaidia vijana kujiendeleza zaidi  pamoja na kuongeza  juhudi za ujenzi wa viwanda kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza uchumi.

Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao watanufaika na profamu hiyo akiwemo Saimoni Nyimmba pamoja na Joseph Bada wamesema kwamba  mafunzo hayo ya kilimo na maarifa  pindi watakapomaliza yataweza kuwasaidia  kuwapatia  kipato pamoja na kuachana na suala la kuwa tegemezi  sambamba na  kuondokana na kile kilimo cha kizamani.

MAFUNZO hayo ya kilimo na maarifa yataweza kuwanufaisha vijana wapatao 200 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambapo kwa sasa yataanza kuwanufaisha vijana 62 kutoka katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo ujuzi watakaupata wataweza kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.