Mkaa mgandamizo ni mchnganyiko maalum wa taka za majani, vumbi ya mbao au mkaa, pumba za mchele na aina nyinginezo za tungamotaka (Biomass). Mkaa mgandamizo unatumika kama nishati mbadala katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
FAIDA ZA MKAA MGANDAMIZO.
Kwa kuwa mkaa mgandamizo hutenngenezwa kwa kugandamiza mchanganyiko wa nishati mbalimbali na/au tungamotaka unakuwa mgumu na uliogandamana hivyo unapowaka unatoa joto kali.
Unawaka taratibu na kwa muda mrefu kutokana na mchakato wa ugandamizaji.
Ubora wa hali ya juu. Mkaa mgandamizo ni zaidi ya asilimia 50 kwa ubora kulinganisha na kuni au mkaa wa kawaida. Una joto zaidi na unawaka muda mrefu zaidi.
Hauna kero ya moshi na ni salama zaidi.
Hauna kero ya moshi na ni salama zaidi. Hauzalishi sumu hatarishi kama Sulphur au CO.
Malighafi kwa uzalishaji inapatikana kirahisi bila kuleta athari yoyote ya uharibifu wa mazingira.
Ni rahisi katika utunzajina usafirishaji.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.