ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 9, 2016

MKOA WA MWANZA UKO TAYARI KUMPOKEA RAIS MAGUFULI.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
 RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli akiwa njiani kesho siku ya Jumatano ya tarehe 10, akitokea mkoani Geita atahutubia wakazi wa vijiji na viunga vilivyoko maeneo ya kando kando mwa barabara kuu hadi wilayani Sengerema na baadaye kuelekea jijini Mwanza kwa mapumziko.

Siku inayofuata Alhamisi ya tarehe 11, majira ya saa 7 mchana, Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Furahisha pamoja na kukagua ujenzi unaoendelea wa barabara iendayo uwanja wa ndege wa Mwanza yenye urefu wa kilomita 2.7 na kisha baadaye majira ykuhutubia wananchi katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya kikazi mkoani Mwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015, tarehe 29 mwezi March, Mhe. Dkt. Magufuli alitua Mwanza na kuishia uwanja wa ndege ambako alitoa maagizo na kisha akala na uwanjanni hapo kisha kuelekea kijijini kwake Chato mkoani Geita.

WAKATI HUO HUO.
Wanamuziki watakao tumbuiza kwenye mkutano wa Magufuli katika viwanja vya Furahisha Mwanza hii leo wametembelea studio za Jembe Fm Mwanza kuzungumzia tumbuizo zao katika kusanyiko la siku ya Alhamisi (tarehe 11 August 2016).

Christian Bella, na JJ Band ikiwakilishwa na January Eleven pamoja na Abby Solo wamejikita leo katika kipindi cha Kazi na Ngoma kuelezea kazi zao sanjari na kile watakachokifanya siku husika.
Wasanii wa muziki Tanzania Christian Bella toka Malaika Band (kushoto) akiwa na January Eleven wa JJ Band ndani ya studio za Jembe Fm hii leo kwa mahojiano.
Ndani ya Jembe Fm kipindi Kazi na Ngoma.
Christian Bella amelazimika kuweka saini kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Alliance Academy Mwanza baada ya wanafunzi hao kumtaka afanye hivyo.
Watu na watu wao zoezi likiendelea.
January Eleven wa JJ Band na saini kwa mashabiki wake.
Christian Bella katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Alliance Academy Mwanza ndani ya studio za Jembe Fm.
Mtangazaji wa kipindi cha mchana kiitwacho Hit Zone, Natty E Brand akipata u-Foto na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Alliance Academy Mwanza
Mwalimu na wanafunzi wake shule ya Sekondari ya Alliance Academy Mwanza

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.