WATU zaidi ya 200 wakiwemo watoto wadogo , wakinamama, wazee, pamoja na vijana katika halmashauri ya mji mdogo Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamefanyia upasuaji wa macho baada ya kugundulika wana matatizo ya ugonjwa ujulikanao kama mtoto wa jicho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kilele cha zoezi hilo la upimaji wa macho bure lililofanyika katika shule ya msingi Bwilingu baadhi ya wananchi hao waliopatiwa matibabu akiwemo Asha Abdalah,Retisia Msangi pamoja na Iddy Chuma walisema kwamba hapo awali walikuwa wanasumbuliwa na tatizo la kuona lakini kwa sasa wamepatiwa matibabu ambayo yameweza kuwasaidia hata katika kuona na kusoma maandishi.
Walibainisha kuwa ugonjwa huo wa macho umekuwa ukiwasumbua kwa kipindi kirefu lakini walikuwa wanashindwa kwenda hospitali kupatiwa huduma ya matibabu kutokana na gharama yake kuwa ni kubwa lakini wanashukuru kupatiwa huduma hiyo bila ya malipo yoyote.
“Tunashukuru kwa juhudi zinazofanywa na Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete kwa kuweza kutujali wananchi wake katika suala la afya, kwani tuneweza kupima macho na kupatiwa matibabu ya aina mbali mbali ikiwemo upasuaji,kupewa dawa na wengine tumepatiwa miwani ya macho hilli jambo tunashukuru na tunaiomba serikali nayo iweze kutusaidia zaidi maana baadhi ya wenzetu wameweza kupata upofu,”walisema.
Kwa upande wake Mratibu kutoka Taasisi ya macho ya Bilal Muslim Mission Ain Sharif alisema kwamba katika uendeshaji wa zoezi hilo wamewafanyia upasuaji wagonjwa zaidi ya 200 pamoja na kuwapatia matibabu ya dawa na miwani zaidi ya wagonjwa 3000 ambao baadhi yao amedai wangecheleweshwa wangekuweza kupata upofu.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa mwisho kushoto akiwa na baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakijadili jambo kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo vya afya |
“Mimi kama mbunge wenu nitaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha kwamba sekta ya afya inaboreshwa katika maeneo mbali mbali kuanzia ngazi za vijijini lengo ikiwa ni kwa ajili ya kila mwananchi aweze kupata huduma ya matibabu ambayo inastaili sambamba na kuongeza wauguzi pamoja na madaktari,”alisema Ridhiwani.
Aidha katika hatua nyingine aliwahimiza wananchi wa jimbo la chalinze kujenga utaratibu wa kwenda kupima afya zao mara kwa mara hususan ugonjwa wa macho ili kuweza kujua kama wana matatizo yoyote ambayo yanaweza kupelekea kutokuona vizuri.
WANANCHI 3500 katika halmashauri ya mji mdogo wa Chalinze Wilayani Bagamoyo wamepimwa na kubainika na kuwa na matatizo mbali mbali ya ya ugonjwa wa macho na kupatiwa matibabu ya dawa, kupewa miwani na wengine kufanyiwa upasuaji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.