ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 12, 2016

NAIBU WAZIRI Mh. ANGELINE MABULA ATEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU

Mh. Angeline Mabula (Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela) akionyesha ufundi wa kucheza mpira wa kikapu katika kituo cha mafunzo kwa watoto Katika mchezo wa mpira wa kikapu kilichopo Kiloleli Katika manispaa ya Ilemela. Kituo hiki hufundisha watoto wa shule za msingi na sekondari mchezo huu ambapo kina zaidi ya watoto 100 wanaohudhuria program ya mafunzo haya ambayo ilianza toka mwezi May mwaka huu.
Ugawaji wa vifaa ulifuata.
Vifaa madhubuti kwaajili ya mpira wa kikapu.
Hii ni hamasa tosha kwa watoto hasa wenye umri huu mdogo, ambapo hujijengea fikra na kuuthamini mchezo toka damuni.
Mkono wa kheri toka kwa mama Mh. Angeline Mabula (Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela) akiutoa kwa moja kati ya vijana wanao fanya vyema ndani ya kituo hiki cha kufundisha watoto wa shule za msingi na sekondari mchezo mpira wa kikapu aka Basketball.


MH. ANGELINE MABULA ATEMBELEA KITUO CHA KUKUZIA VIPAJI KWA WATOTO KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU CHA KILOLELI MWANZA.

SIKU ya tarehe 9 julai 2016, Mh. Angeline Mabula (Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela) ametembelea kituo cha mafunzo kwa watoto Katika mchezo wa mpira wa kikapu kilichopo Kiloleli Katika manispaa ya Ilemela. Kituo hiki hufundisha watoto wa shule za msingi na sekondari mchezo huu ambapo kina zaidi ya watoto 100 wanaohudhuria program ya mafunzo haya ambayo ilianza toka mwezi May mwaka huu.

Pamoja na kutembelea kitu hiki, Mh. Angelina Mabula ambaye pia alishawai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha  Mpira wa Kikapu Mkoa Mwanza (MRBA) pia mweka hazina wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), alikabidhi jezi jozi (pair) 3 kwa wanafunzi wachezaji waliofanya vizuri Katika mitihani yao ya kufunga shule muhula wa kwanza katika shule zao, pia wengine 2 watapatiwa dhawadi zao siku ya uzinduzi wa program hii utakaoambatana na bonanza la mchezo huu kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Ilemela na Nyamagana.

Wanafunzi hao ni Nestory Michael na Lubango Michael wa darasa VI shule ya msingi Pasiansi, Jackso Shadrack wa DRS V Pendo Eng. Medium na wanafunzi watakaopata zawadi zao baadae ni Carlos I. Benjamin wa DRS VII shule ya msingi Pasiansi na Alifa Jamal wa Kilimani sec School kidato cha III. Wanafunzi hawa wamepata zawadi hizi mara baada ya kuahidiwa kwa washiriki wote kuwa, kwa yeyote atakayefanya vizuri Katika mitihani yake shule atapata zawadi, hii ni kuwataka watambue kuwa kucheza na kusoma huenda pamoja.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa fupi kwa Mh. Angeline Mabula, Mratibu wa program hii, Kizito Sosho Bahati, alisema, tunalenga kuinua mpira wa kikapu mwanza kama ilivyokuwa awali na kuwa na wachezaji mahili wataokuwa wakicheza na kuiwakilisha Mwanza Katika mashindano mbalimbali na kufanya vizuri. Kwani Katika miaka ya nyuma timu za Mwanza Katika mashindano yeyote kwa ngazi tofauti tofati zilifanya vizuri sana kiasi cha kupelekea wachezaji wengi kusajiliwakatika timu nyingi za mkoa wa Dar es Salaam.

Pamoja na kukubali kuja kuwa mgeni rasmi siku ya uzinduzi rasmi utakaofanyika siku ya jumamosi ya tarehe 16 July 2016, Mh. Angeline amehaidi kusaidia program hii na pia kuangalia namna ya kuongeza michezo mbalimbali Katika mashindano ya Jimbo Cup yatakayokuja fanyika siku zijazo.
IMETOLEWA:

KIZITO SOSHO BAHATI
MRATIBU WA MAFUNZO

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.