Serikali ya China imeichagua Tanzania kuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa mpango wake wa kuhamishia viwanda barani Afrika katika kipindi ambacho Tanzania nayo imekuwa ikihamasisha ujenzi wa viwanda kama msingi na mhimili mkuu wa uchumi.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema hayo wakati wa semina ya siku moja ya kimataifa, iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini ambapo amesema serikali imetenga kiasi kikubwa cha bajeti kwenda kwenye miundombinu kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa viwanda.
"Tumesikia katika semina hii kwamba wenzetu Wachina wameichagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutekeleza mpango wake wa kuhamishia viwanda barani Afrika, hii ni fursa nzuri kwetu ambapo kama serikali tumeamua kutenga zaidi ya asilimia arobaini ya bejeti kwenda kwenye miundombinu kwa ajili ya kuchochea kasi ya uanzishaji wa viwanda," amesema Profesa Mbarawa.
Amefafanua kuwa kupitia miundombinu bora, kutakuwa na kasi ya uanzishwaji wa viwanda kwani wakulima watapata urahisi wa kusafirisha mazao yao sambamba na kuwa na uhakika wa bidhaa kufika sokoni na hivyo hivyo kwa malighafi kwenda viwandani.
Semina hiyo imewakutanisha wataalamu wa uchumi na viwanda kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo nguli wa masuala ya uchumi Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ameshauri kuwepo na upatikanaji wa nishati ya uhakika, elimu bora kwa vijana ambao mwishowe ndiyo watakuwa waajiriwa wa viwanda hivyo.
"Taarifa zinaonyesha kuwa China hivi sasa inaachana na viwanda vinavyoajiri watu wengi na badala yake wanaanzisha viwanda vinavyotumia teknolojia za kisasa..hii ni nafasi nzuri kwa nchi kama Tanzania kwani kuna kila dalili viwanda vinavyoajiri watu wengi vitakuja nchini na hii ni angalizo kwamba tujiandae kuwa na wataalamu watakaoajiriwa katika viwanda hivyo ili sehemu kubwa ya mapato ibaki hapa hapa nchini," amesema Profesa Lipumba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Godfrey Simbeye ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambapo katika mahojiano na EATV amesema wameandaa kongamano la siku tatu litakaloanza Agosti 17 mwaka huu kama moja ya hatua za kuitikia wito wa serikali kuhusu viwanda.
Kwa mujibu wa Simbeye, kongamano hilo litakutanisha wadau na wamiliki wote wa viwanda kwa lengo la kuangalia ni namna gani wito wa serikali wa kuchangamkia
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.