Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Henry Makale, mapema leo ofisini kwake. PICHA NA GSENGO BLOG |
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa TAKUKURU mkoani hapa Henry Makale amesema kuwa Taasisi hiyo inaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na pindi utakapokamilika Mkurugenzi pamoja naAfisaUtumishi wa Jiji la Mwanza watachukuliwa hatua za kisheria kwa kushindwa kuwasilisha majina ya watumishi hao hewa.
Yote haya yanajiri ikiwa ni siku moja baada ya Halmashauri ya jiji la Mwanza kudai kuwa haina watumishi hewa bali wafanyakazi watoro wapatao 60.
Kamanda Henry ameeleza jinsi walivyobaini mchezo mchafu unaofanywa na Halmashauri hiyo. "Tayari tumebaini kuna uongo ambao huwa unafanywa na Halmashauri hizi kuwasilisha wafanyakazi hewa, Orodha ya majina yaliyowasilishwa kwa mkuu wa mkoa haina majina yote kwamaana tumefanya uchunguzi wa awali Halmashauri ya Jiji na kubaini kuwa kuna wafanyakazi wa 5ambao hawakuwasilishwa kwenye orodha iliyopelekwa kwa Mkuu wa Mkoa"
"Lakini tumeamini Halmashauri husika wanawafahamu kwasababu ni majina ya wafanyakazi hewa lakini pia yamekopewa kwenye mabenki mbalimbali" akaongeza kuwa " Wametumia waraka feki, wamegushi nyaraka kwa maana ni watu wenye nafasi kubwa na kwa kweli Serikali haina simile kwa hili" alisema Kamanda wa TAKUKURU Mwanza, Henry Makale.
Kufuatia hali hiyo TAKUKURU imetoa Onyo kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza ambapo zoezi hilo linaelekea, ikiwatahadharisha wakuu wote na wasimamizi wa Idara na vitengo husika kutoa takwimu sahihi bila kupepesa macho.
Kipindi cha mwezi January hadi March mwaka huu TAKUKURU imeweza kupokea malalamiko 27 kuhusu vitendo vya rushwa huku idara zinazo lalamikiwa ni pamoja na Ardhi, Mahakama, Polisi na Afya.
Aidha kwa kesi zilizofikishwa mahakamani kwa kipindi hicho TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imefikisha watu 9 mahakamani akiwemo aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata na wenzake Justine Bilindaya Lukaza aliyekuwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela na Mfanyabiashara Hemed Hamad Hemed kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya umma kwa kutoa zabuni ya kutoza ushuru katika stendi ya mabasi ya Buzuruga kinyume na Utaratibu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.