Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Tanzania Dar es Salaam , (PICHA PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene katika Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Tanzania Dar es Salaam leo
Baadhi ya wafanya biashara wakinyoosha mikono mara walipoulizwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Tanzania, Johnson Minja niwangapi wangempa kura Rais Magufuli kama leo ingekua ni uchaguzi?
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akizungumza akiagana na wafanya Biashara mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Tanzania Dar es Salaam leo.
Khamis Mussa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, ameifuta bodi ya uongozi ya jengo la wafanyabiashara la Machinga Complex kutokana na kwamba uongozi huo kushindwa kufanyakazi inavyotakiwa.
Hatua hiyo imefikiwa Dar es Salaam leo ambapo Waziri aliweka wazi kuwa kwa sasa jengo hilo litasimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda kwani umiliki uliokuwepo ni batili na hauna tija kwa taifa.
Akitangaza uwamuzi huo wakati akizungumza katika mkutano wa taifa wa wafanyabiashara, alisema kuwa watumishi wote na meneja anaesimamia jengo wameshindwa kazi na kwamba arudishwe katika ofisi za jiji ili apatiwe kazi nyingine.
Pamoja na kutangaza kuwa uongozi huo kuwa batili lakini aliweka wazi kuwa hata mikataba yake ni batili katika taifa, kwani umewatenga wananchi waliotakiwa kunufaika kutonufaika kutokana na baadhi ya watu kufanya mambo yao kwa kujinufaisha wao wenyewe.
"Uongozi na mikataba ni batili kwani umetenga watu ambao walitakiwa kunufaika kutonufaika hivyo natangaza kufuta kila kitu na kuanzia leo namtangaza mkuu wa mkoa kuwa 'inchaji' wa eneo hilo," alisema.
Alisema kuwa eneo hilo halitaweza kuachwa na kuchezewa hivyo na kuutaka uongozi kutafuta utaratibu mpya wa kuwaingiza wafanyabiashara wafanyebiashara na taratibu za ulipiaji kuanza baadae.
Aliweka wazi kuwa jengo hili liligharimu sh.bilioni 12.7 ambazo zilikopwa NSSF, lakini chakushangaza hadi leo zimelipwa sh.milioni 50 tu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.