MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya kuwa na tamaa ya kuwaozesha watoto wao kike mapema huku wakiwa na umri mdogo na badala yake wahakikishe wanatilia mkazo zaidi ya kuwaendeleza katika elimu na sio vinginevyo.
Ndikilo ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo,pamoja na watendaji kuhusiana na kujadii changamoto iliyopo ya kuwepo kwa ongezeko la ndoa za utotoni ambazo zimeonekana kuwa ni kikwazo kwa baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo yao.
Amesema kuwa katika Mkoa wa Pwani anasikitishwa sana kuona baadhi ya wazazi wanafanya mambo kinyume kabisa na sheria kwani wanaamua kuwaozesha watoto wao kwa watu wazima waliowazidi umri kutokana na tamaa zao za kujipatia pesa kwa urahisi bila ya kuangalia madhara yake.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwamba tatizo la ndoa za utotoni linaathiri kwa kiwango kikubwa kuzolota kwa kiwango cha elimu,hasa kwa motto wa kika afya ya uzazi pamoja kuwepo kwa ushiriki hafifu katika shughuli za uzalishaji na uongozi.
SIKILIZA
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii mkoani Pwani,Asha Itelewe,amesema kwamba hali ya ndoa za utotoni bado ni changamoto hali ambayo inaonyesha kwa kipindi cha mwaka jana katika mkoa huo ilikuwa ni asilimia 33 huku kitaifa ikiwa ni asilimia 35.
MSIKILIZE AFISA MAENDELEO
Katika hatua nyingine akizungumzia kuhusiana na changamoto kubwa iliyopo katika sheria ya ndoa hapa anafafanua zaidi.
AFISA
Tafiti za mwaka jana zilizofanywa na wizara ya afya mkoani hapo zinaonyesha masuala ya ndoa za utotoni ni asilimia 33 huku masuala ya ukeketaji ni asilimia 10 hivyo ni jukumu la jamii kushirikiana na wadau na serikali kupunguza tatizo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.