NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KUNDI jipya linalokuja kwa kasi katika miondoko ya muziki wa mduara hapa nchinini la( MTP) lenye maskani yake eneo la maili moja Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeachi wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Kavimba jicho.
Akizungumza na Tanzania daima Mkurugenzi wa kundi hilo Mudy Mnembwe alisema kwamba maandalizi yote kwa ajili ya nyimbo hiyo tayari yamekwsiha kamilika na kwamba wimbo huo unatarajiwa kuanza kusikika hivi karibuni katika vituo mbali mbali vya redio.
Mnembwe alisema kwamba nyimbo hiyo ambayo inavionjo vya mduara vilivyomo katika wimbo huo ana imani vitaweza kuwa kivutio kikubwa na gumzo kwa mashabiki wa wao kutokana na ujumbe uliomo ndani yake pamoja na mpangilio wa sauti umepangiliwa kwa staili ya kipekee. BOFYA PLAY KUSIKILIZA
“Ndugu mwandishi kwa sasa kundi letu baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha muda mrefu tumekuja upya na maadhi ya mduara kwa hiyo wimbo huu mpya kwa upande wangu utaweza kukonga nyoyo za mashabiki wetu kwa hiyo wakae mkao wa kula kuusikiliza katika stesheni mbali mbai za redio kwani tumeshaanza kuusambaza na umerekodiwa katika studio ya Mauntain za mjini Kibaha ,”alisema Mnembwe.
Aidha Mnembwe alisema kuwa katika wimbo huo mpya wameamua kuwashirikisha wasanii ambao wanachipukia katika anga ya muziki kutoka Mkoa wa Pwani pamoja na wasanii wengine ambao tayari majina yao ni makubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Aliwataja wasanii hao ambao wameshiriki kikamilifu katika wimbo huo ni pamoja na Eli Dadi, Mapesa, Maph, Nash, Dee Dollarz, pamoja na mwana muziki wa siku nyingi katika muziki wa kizazi kipya Spark ambaye alishawahi kufanya vizuri katika nyimbo zake.
Pia katika hatua nyingine Mnembwe alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anatumia fursa kwa vijana ambao ni wazawa wa Wilayani Kibaha wenye vipaji na kuweka kuweka mikakati endelevu ya kuwainua na kuwaendeleza zaidi katika muziki wa aina mbali mbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.