Thursday, April 21, 2016
HABARI
Mtazame Hapa Alivyokuwa anamwaga cheche:
Katika hali inayoonyesha kuwa na majibizano kati ya Rais Magufuli na Kituo Cha Haki za Binadamu LHRC kinachoongozwa na Dr. Hellen Kijo Bisimba, leo Rais Magufuli hadharani kasema wanaosema amekiuka haki za binadamu kumsimamisha ndugu Kabwe hadharani walitakiwa pia waseme vivyo hivyo kipindi anamuapisha hadharani kwa kuwa ni mteule wake.
Amesema hao Waliotumbuliwa wamewaibia Watanzania hadharani hivyo inabidi watumbuliwe hadharani nao wapate maumivu kama waliyoyapata Watanzania...Hivyo, ni vyema wakaiacha serikali ikafanya kazi yake, na ikiwezekana itabidi awachunguze hao LHRC credibility yao kama wanatetea mambo maovu inawezekana nao ni majipu..
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.