NA VICTOR MASANGU,
GSENGO BLOG PWANI.
JESHI la polisi Mkoa wa Pwani limemkamata na kumfikisha mahakamani Afisa Tarafa wa Kibiti Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Selemani Mpangile almaarufu babu konyeza kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi kitunda.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushogi amesema kwamba tukio hili limetokea juzi majira ya saa 10 jioni ambapo mtuhumiwa aliamua kutenda kosa hilo kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Mushongi alisema kwamba jeshi la polisi litaendelea kuvalia njuga vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo kwani kunaweza kuwasababishia madhara makubwa watoto hao kutokana na kufanyiwa vitendo kama hivyo wakiwa na umri mdogo.
Kamanda Mushongi amefafanua kuwa tukio hilo la ubakaji mtuhumiwa alilifanya katika ofisi yake wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akipita nje ya jengo hilo na ndipo alipomwita na kuingia ndani ambapo alimziba mdomo wake kwa koti leke ili asipige kelele kasha kutekeleza azma yake ya kumbaka .
Katika hatua nyingene Kamanda ametoa onyo kwa wanafunzi kuachana na tabaia ya kuwa na tamaa ya kupenda vitu vya bure, na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawatunza na kuwalea watoto wao katika misingi mizuri ya kimaadili na sio kuwa na fikra potofu.
“mimi napenda kutoa onyo kwa wanafunzi na watoto waache kabisa tabia ya kuwa na tama, kwani wakifanya hivyo matokeo yake ndio hayo kwani wakati mwingine wanapenda vitu vya bura kama pipi, soda kwa hivyo hii ni hatari sana, pia na wazazi wahakikishe wanawalinda watoto wao,” alisema Mushongi.
MATUKIO ya vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Pwani bado yanaonekana kuwa ni tatizo kubwa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi zifanyike na serikali katika kuwachukulia hatua kali za kisheria na kutoa adhabu kali kwa wale wote watanaobainika kuhusika katika matukio kama hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.