Mwanamuziki kutoka Marekani maarufu kwa muziki wa chapa Funk, Prince ameaga dunia.
Mwanamuziki huyo raia wa Marekani alipatikana ameaga dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis. Alikuwa na umri wa miaka 57.
Prince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na themanini kwa vibao vyake maarufu kama vile 'I Wanna Be Your Lover' na 'Little Red Corvette'.
Anasifika kwa ubunifu wake wa kutajika na kwa midundo iliyowaongoa wapenzi wa muziki kote duniani .
Prince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia''.
Muziki wake ulikuwa maarufu kiasi ya kwanza aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100.
Kipawa chake kilimwezesha kutunga kusanifu kutayarisha na pia kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Vile vile aliwatungia nyimbo waimbaji wengi tu kote duniani.
Yamkini msanii huyo nguli alikuwa anaugua kwa kipindi kirefu na hata alilazimika kukatiza Shoo zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.
CHANZO BBC SWAHILI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.