Hatimaye Atletico Madrid imeng'ara katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliopigwa usiku wa leo Jumatano wakati timu hiyo ikipepetana na Bayern Munchen Jijini Madrid katika uwanja wa Estadio Vicente Calderon.
Goli la Saul Niguez alilofunga kunako dakika ya 11' kipindi cha kwanza lilidumu hadi mapumziko na hata tamati ya mchezo huo.
Kwa ushindi huo mwembamba wadau mbalimbali wa michezo ulimwenguni wamekuwa wakiuangalia mchezo huo kama ni bado mbichi kwani Bayern wana uwezo wa kubadili matokeo hayo katika mchezo wa marudiano utakao pigwa Allianz Arena.
Jana Manchester city na Real Madrid zilitoka sare ya bila kufungana.
Mchezo huo ukiwa pia ni wa hatua ya Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kufuatia matokeo hayo Sasa timu hizo zitarudiana wiki ijayo katika Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid Hispania katika mchezo wa marejeano.
Fainali ya Michuano ya hii itapigwa Jumamosi tarehe 28.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.