BBC SWAHILI:-
Timu za Real Madrid na Vfl Wolfsburg zimekua timu za kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya.
Real Madrid wakicheza katika dimba lao la Santiago Bernabeu wameibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya As Roma, mabao ya timu hiyo yakifungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga bao lake la 40 kwa msimu huu, na bao la pili likifungwa na James Rodriguez.
Madrid wanasonga mbele wakiwa wamepata ushindi wa mabao 4-0 ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Itali walishinda kwa mabao 2-0.
Nao Wajeruman wa Vfl Wolfsburg wamesonga mbele kwa kuwachapa Kaa Gent kwa bao 1-0 bao lilofungwa na mshambuliaji Andre Schurrle, katika mchezo wa wa kwanza Wolfsburg walishinda kwa mabao 3-2.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.