Bring back our Salma Said
Ungana na Wanahabari kupaza sauti kurejeshwa kwa Mwandishi wa DW na Gazeti la Mwananchi Bi. Salma Saidi..aliyetekwa na watu wasiojulikana na kuwekwa kizuizini nchini Tanzania
|
Kumekuwapo na taarifa zinazoripotiwa kwa vyombo vya habari za kuhusu kutekwa kwa mwandishi wa habari wa Sauti ya Ujerumani Zanzibar (DW), ambaye pia ni mwanahabari wa gazeti la Mwananchi la hapa Tanzania, Bi. Salma Said (pichani) ambaye ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam. Tunaamini hali hii si nzuri kwa mwanahabri mwenzetu na inaleta machungu na fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake kwa kipindi hichi kigumu.
Mtandao huu wa Modewjiblog unaungana na Wanahabari wote kokote pale walipo na familia ya Bi. Salma kuweza kupaza sauti ili mwenzetu aweze kupatikana ama kuachiriwa huru.
Hatuamini watu hao waliomteka mwanahabari kuwa wana nia gani ila, tunaomba kwa Idara husika ikiwemo Serikali ambayo inajukumu la kulinda raia na mali zake kulifanyia kazi suala hili bila kuingilia utaratibu mwingine.
BRING BACK OUR SALMA SAID
BRING BACK OUR SALMA
BRING BACK OUR SALMA
TUNAOMBWA KUACHIRIWA HURU KWA MWANAHABARI SALMA SAIDI.
Ukiwa mwanahabari, Mwanajamii na mtanzania mpenda Amani, ungana katika kupaza sauti ya kurejeshwa kwa Mwanahabari Salma Saidi! Kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine yoyote ile ilikusikika kwa sauti yako.
Bring back our Salma Said. Bring back our Salma Said Kusoma zaidi matamko ya habari hizi bonyeza hapa: http://dewjiblog.com/2016/03/20/utpc-yatoa-tamko-kuhusu-kutekwa-kwa-mwandishi-wa-dw-salam-said/
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.