Hakuna kampuni nyingine nchini inayotoa huduma kama hiyo zaidi ya Smile.” AliongezeaBw. Behner.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Smile Unlimited, Bw. Behner amesema kuwa huduma hiyo ipo ndani ya sera ya kampuni ya usawa katika matumizi.
Sera hii itamfaidisha mteja kwani itamuhakikishia kuwa anakuwa ameunganishwa kwa uhakika ndani ya siku zote 30.
Programu ya SmileVoice app inawawezesha wateja ambao hawana simu za VOLTE uhakika wa kupiga simu kupitia mfumo wa LTE wakiwa wameunganishwa na mtandao wa intaneti wa Smile.
“Katika soko la Tanzania, watu wenye vifaa vinavyo tumia Android ndivyo vinavyo ongoza na ukijumlisha na SmileVoice app, basi tuna wahakikishia wateja wetu watakaosajili nasi watajionea na kujivunia upigaji simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia simu zao.” AliongezeaBw. Behner
Ili kuweza kutumia huduma ya Smile Voice, inambidi mteja awe na SIM iliyosajiliwa na akiwa na kifurushi cha Smile.
Programu hii inaweza kupakuliwa (downloaded) kwenye simu zinazo tumia mfumo wa Android na za iPhone (IOS) na hufanya kazi mara tu baada ya mteja kujisajili nayo mara moja.
Wakati simu ikiwa haina intaneti ya mtandao wa Smile mteja anaweza kupiga simu kwenda simu nyingine ambayo imeunganishwa na mtandao wa intaneti wa 3G, Wi – Fi au nje ya nchi. Mwisho ….
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.