ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 13, 2015

MAADHIMISHO YA UHURU NA USAFI 2015 YAIACHA ILEMELA PABAYA.

Uhuru na Usafi ikiwa ni Kauli mbiu ya maadhimisho ya UHURU wa Tanganyika (Tanzania bara)  ambayo yalikuja kupitia amri ya Amiri jeshi mkuu wa nchi yetu Dkt John Pombe Magufuli kuzitaka familia na taasisi nchini kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi tofauti na vile ilivyozoeleka kwa kupiga gwaride na hotuba viwanjani. Lakini maadhimisho hayo hayajawa na manufaa kwa wananchi na wakazi wa Ilemela Mwanza.
Baada ya Maadhimisho ya Uhuru kufana na hata kiasi cha idadi kubwa ya wananchi kuomba zoezi hilo kuwa endelevu ...sasa licha ya wananchi wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wakiongozwa na Mbunge wao kuitikia kwa kiwango cha juu kutekeleza zoezi hilo, kwa kusafisha makazi yao, mifereji na mitaro ya barabara, chakusikitisha ni kuona hadi LEO taka walizo kusanya ili zizolewe, hazijasombwa na magari ya taka ......
Taka hizo sasa zinarudi kwenye mifereji pembezoni mwa barabara....MMMMMMMmmmmm!!!
Ni mwendo kufukia mitaro...Na kama ni zoezi la usafi tuanze moja.
Hapo vije..??
Ni barabara ile ile ya Kilimahewa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Wadau husika hamuoni au mmeenda kunya chai? 
Nini tatizo?
NAOMBA KUWASILISHA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.