ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 7, 2015

CCM MWANZA YATEUWA WAGOMBEA NAFASI ZA WENYEVITI NA MAKAMU WENYEVITI HALMASHAURI SITA MKOA WA MWANZA KATI YA NANE

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa, Saimon Mangelepa.
Na PETER FABIAN, MWANZA.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza jana kiliketi na kimeteuwa Madiwani kugombea nafasi ya Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya sita kati ya nane za Mkoa wa Mwanza.
 
Akizungumza na wandishi wa Habari jana katika Ofisi za Chama mkoani hapa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa, Saimon Mangelepa, alisema kwamba uteuzi huo umefanywa na Kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa baada ya Kamati za Siasa Wilaya kuchuja na kuwasilisha mapendekezo ngazi ya Mkoa ambapo iliyapitia na kisha kuteuwa wagombea waliokidhi sifa.
 
Mangelepa alisema kwamba Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dkt Anthony Dialo, ilipitia majina ya wagombea kutoka Halmshauri za Wilaya Nane lakini imeteuwa wagombea kutoa Halmashauri sita ambazo ni Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema, Buchosa, na Ukerewe.
 
Kamati hiyo pia ilipitia na kupendekeza majina ya wagombea nafasi ya Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela ambapo mapendekezo hayo yamepelekwa Kamati Kuu ya Chama hicho Taifa ambacho kinaketi leo kujadili na kuteuwa wagombea nafasi za Mameya na Manaibu Meya wa Halmashauri za Majiji na Manispaa nchini kote.
 
“Majina ya Meya na Manaibu Meya wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela huteuliwa na Kamati Kuu Taifa ya CCM hivyo Kamati ya Siasa Mkoa haina mamlaka nayo zaidi ya kupitia tu na kupeleka mapendekezo hayo ngazi hiyo ambayo kesho (leo) itakaa na kufanya uteuzi wake na majina hayo yatatangazwa na Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa , Nape Nnauye (Mbunge wa Mtama),” alisema.
 
Mangelepa alizitaja Halmashauri na majina ya wagombea nafasi za Wenyeviti na Makamu Wenyeviti waliopitishwa na Kamati ya Siasa Mkoa, Halmashauri ya Wilaya ya Magu nafasi ya Mwenyekiti walioteuliwa ni Madiwani, John Bunyanya, Elisha Hilali na Malaki Lupondije nafani ya Makamu Mwenyekiti ni Madiwani, Velina Makwandi, Gerald Paul na Faustine Makigi.
 
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi walioteuliwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Madiwani, Bahebe Masele, Bernard Polycarp na Mwamba Makune, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Madiwani, Kiganga Saimon, Mayila Maguha na Jojo Abed. Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba nafasi ya Mwenyekiti ni Madiwani, Majaliwa Mbassa, Ngassa Lucas, Peter Misalaba nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Madiwani, CheyoTendegesa, Malecha Martine na Ntwale James.
 
Mangelepa alizitaja Halmashauri zingine kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambapo nafasi ya Mwenyekiti walioteuliwa ni Madiwani, George John, Kadinda Masasi na Yanga Makaga, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Madiwani,Bulapilo Bikwija, Kiganga Alex na Sengerema Ndekeja,  Halmashauri ya Buchosa (Sengerema) walioteuliwa nafasi ya Mwenyekiti ni Madiwani, Kalunga Saadalahh, Kanyumi Henry.
 
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti walioteuliwa ni Madiwani, Kibinzi Idama na Mashimba Isack, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe nafasi ya Mwenyekiti ni Madiwani, Joshua Manumbu, Nicholaus Mnyoro na George Nyamaha, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Madiwani, Sospeter Mgaya, Gabriel Gregory na Mussa Malima.
 
Mangelepa alisema kwamba wagombea hao walioteuliwa watapigiwa kura kwenye vikao vya Madiwani wa CCM kumpata mgombea mmoja katika kila nafasi ambaye atashindana na wagombea wengine kutoka vyama vya siasa ambavyo vilifanikiwa kupata madiwani katika Halmashauri za Wilaya kwenye Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu lakini ni matarajio yetu CCM itashinda na kuongoza Halmashauri zote nane Mkoa wa Mwanza .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.