WAZIRI mwenye ushawishi mkubwa
katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya
shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na
tuhuma za ufisadi.
Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa
Mipango na Ugatuzi, ameambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na
daktari wake “achukue muda kupumzika”.Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema. CHANZO BBC SWAHILI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.