ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 23, 2015

CHADEMA WAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KANDA YA ZIWA.

Ulinzi umeimarishwa barabara inayoingia mahala penye ofisi za Chadema \mkoa wa Mwanza, jeshi la polisi limefunga barabara hiyo tangu majuzi.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  LEO asubuhi kimetinga katika Mahakama ya Kuu Kanda ya Ziwa jijini Mwanza, na kufungua kesi kutaka kupewa ufafanuzi wa suala hilo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia hatua ya Jeshi la Polisi kuzuia kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo , shughuli ambayo ilipangwa kufanyika katika viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza.
G. Sengo akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu amezungumza na Jembe Fm LIVE asubuhi ya leo BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Mvutano wa shughuli za kuaga mwili wa Mawazo ulijitokeza baada ya polisi mkoani hapa kupiga marufuku shughuli hiyo kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu. Hadi sasa mwili huo umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Mwanza.


Amri hiyo ya kupiga marufuku ilitolewa Ijumaa na kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo aliyesema wamezuia mikusanyiko kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Jana Polisi waliondoa uwezekano wa viongozi na wanachama wa Chadema kuuchukua mwili na kufanya taratibu za kuuaga.
Pia, amri nyingine kama hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie lakini yeye akidai Mawazo si kiongozi wa kitaifa wala mkazi wa mjini Geita.
Ulinzi umeimarishwa barabara inayoingia mahala penye ofisi za Chadema mkoa wa Mwanza, jeshi la polisi limefunga barabara hiyo tangu majuzi.
Mawazo aliuawa Novemba 14 baada ya kutekwa na kundi la watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM ambao walimshambulia kwa silaha za jadi. Alikuwa mjini Katoro, Geita kuhudhuria kikao cha ndani cha maandalizi ya uchaguzi mdogo kata ya Ludete.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.