NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya upataikanaji wa maji Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvessty Koka amesema kwamba endapo akipata nasafi ya kuchaguliwa atahakikisha anasogeza huduma ya maji katika kila mtaa lengo ikiwa ni kupunguza kero ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wake.
Koka ameyasema hayo wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kampeni kwa wananchi wa mtaa wa mikongoro iliyopo kata ya Miswe pamoja na waanchi wa mtaa wa zegeleni kata ya Visiga ambapo amesema anatambua usumbufu wanaoupata wananchi wake hivyo suala hilo atalitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Mgombea huyo alisema kwamba kwa sasa juhudi zake za kutandaza mabomba makubwa katika jimbo la Kibaha mjini zimeshaanza kuzaa matunda hivyo ana imani endapo mradi huo mkubwa pindi ukikamilika utaweza kuleta mabadiliko makubwa na kuwasaidia wananchi ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji inamalizika.
“Ndugu zangu wananchi adha ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa jimbo langi hilo ninalitambua na wakati nipo madarakani nimlishaanza kufanya mchakato wa kuomba mradi kwa serikali na nilikubaliwa na kwa sasa kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kunufaikamkupaata maji safiu na salama, na hili ndilo lengo langu kubwa kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wangu wa kibaha,”.alisema Koka.
Pia aliongeza kuwa huduma ya maji ni jambo la msingi sana kwa maisha ya binadamu hivyo wanachi wa jimbo la kibaha na maeneo mengine wataweza kunufaika na mradi huo ambao hawatapata tena shida kwani maji yatakuwa yanawafikia katika mitaaa yao bila ya kuwa na usumbufu wowote kama ilivyokuwa hapo awali.
Alifafanua kuwa katika kipindi cha nyuma wananachi wake walikuwa wanateseka sana kupata huduma ya maji safi na salama lakini kwa kipindi hiki cha miaka mitano ilyopita kuna mabadiliko makubwa katika sekta hiyo kwani kuna miradi mingin ya maji amabyo imefanyika na mingine badi inaendelea kufanyika ili kuweza kutekeleza ilani ya chama ya kuboresha huduma ya maji kwa wananchi.
Pia ambali na hilo Koka akusita kuwaeleza wananchi wake wanatakiwa kuwa makini kuakikisha wanailinda miradi yote ya maji sambamba na miundombinu yake kwani imetumia gharama kubwa katika utekelezaji wake hivyo kila mwananchi inapaswa awe mlinzi wa mwenzake.
Akizungumzia suala la watendaji ambao watahujumu miundombinu pamoja na miradi hiyo ya maji ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wananachi wa jimbo la kibaha mjini kuondokana na kero ya upatikanani wa maji amedai haweza kuwavulilia hata kidog na badala yake atawacukulia hatua kai z akisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Kwa upande wao wananchi wanaishi katika kata ya visiga pamoja na miswe ambao hawakutaka majina yao yatajwe walisema kwamba mgombea huyo anaetetea kiti chake katika kipindi chake ameweza kujitahidi kushirikiana bega kwa bega katika kuleta mabadiliko katika kila sekta japo kuna baahi ya watendaji wake ndio wanamwangusha kutokana na kuwa na uroho wa madaraka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.