Picha kutoka maktaba. |
JESHI la Polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia watoto watano kwa kosa la kujihusisha na makosa ya uhalifu ikiwa ni pamoja na ubakaji, uporaji ,utekaji kwa kutumia mapanga matukio ambayo wamekuwa wakiyafanya nyakati za usiku mjini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa upelelezi George Bagyemu amewataja watoto hao kuwa ni Medadi Juma,Thomas Charles,Said Mahamoud,Alex Jonathan na Philbert Kwilasa wote wakazi wa mjini Kahama.
Bagyemu amesema watoto hao wamekuwa wakiwateka watu majira ya saa 1 hadi saa mbili usiku na kuwanyang’anya baadhi ya mali zao ikiwa ni pamoja na pochi,simu, fedha na kuwajeruhi kwa kuwachoma na vitu vyenye nchakali kama vile Nondo, Panga,Viwembe,Visu na Minyororo.
Aidha ameongeza kuwa katika matukio ya mauaji,unyang’anyi kwa kutumia silaha na ubakaji yaliyojitokeza mwezi uliopita baadhi ya watoto hao wameshiriki na kusema kuwa sheria ya watoto ya kuwachapa viboko tu haitendi haki kwani wakikamatwa na kufikishwa mahakamani wakitoka huwa wanaendelea na vitendo hivyo.
Hata hivyo akaitaka jamii kuwalea watoto wao katika misingi bora ya makuzi yao kwa kuwa hata mataifa ambayo yapo kwenye machafuko sasa chanzo chake ni vikundi vya namna hii ambavyo baadae hukua na kuwa makundi yanayohatarisha amani katika jamii duniani kote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.