Tumbuizo za aina yake ambazo ziliweza kukonga nyoyo za waanchama wa CCM, pamoja na wananchi waliofika uwanjani hapo kusikiliza sera za mgombea huyo. |
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba ndapo akichaguliwa na wananchi hatoweza kuwavuila wauguzi na madaktari wenye tabia ya kuiba dawa za serikali kinyume na taratibu na kuamua kuzipeleka katika madukani yao pamoja na wale ambao wanawanyanaya wagonjwa na kuwabagua
Hayo hameyasema wakati wa mkutano wake wa hadhara wa kampeni na wananchi wa kata ya misugusugu ambapo amesema kwanba suala hilo atahakikisha analivalia njuga bila kumwonea aiabu mtu yoyote lengo ikiwa ni kudhitibiti mianya ya wizi wa madawa pamoja na kuboressha huduma ya afaya kwa wagonjwa bila ya kuwa na ubaguzi.
Koka alisema kwamba kuna baadhi ya maeneo ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kumekuwepo na vitendo vya unyanyasaji kwa baadhi ya wagonjwa pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu hivyo ataweza mkakati kabambe wa kushirikiana na watumishi wengine kulisimamia kikamilifu jambo hilo ili kuimarisha sekta ya afya.
“Mimi jamani wananchi wangu ninasikitishwa sana na kuona baadhi ya wauguzi au madaktari wanakuwa hawawatendei haki wagonjwa wakati mwingine wanawabagua na kuwanyanaysa hii kwa kweli mimi kamwe siwezi kuikalia kimya ni lazima nitawashughulikia watu wa aian hiyo kwani ndio wanafanya kuzolota kwa utoaji wa huduma,”
“Mbali na kuwepo kwa hali hiyo katika baadhi ya maeneo pia kuna wengine sasa wanaamua kuvunja sheria na taratibu amabzo zimeekwa kwa kuchukua madawa ya serikali ambayo yamepelekwa kwa ajili ya kuwapatia wagonjwa, ila wao wenyewe wanayachukua na kuyapeleka katika maduka yao binafsi kwa mafunuaa yao badala ya kuwapatia matibabu wagonjwa,”alisema Mgombea huyo kwa masikitiko.
Pia Mgombea huyo alibainsiha kuwa apendi kuona mgonjwa anapokwenda kutibiwa anafanyiwa vitendo ambavyo sio sahihi katika upatikanaji wa kupatiwa matibabu, hivyo wauguzi na madaktari wanapaswa kufanya shughuli zao kwa umakini na uadilifu mkubwa bila ya upendeleo kwa wagonjwa.
Aidha amewaomba wananchi wa jimbo la Kibaha mjni pamoja na Taifa zima kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuhakikksha wanajiunga katika mfuko wa bima ya afya ambao una faida kubwa ya kuweza kuwasaidia kuwapatia matibabu bure pindi wanapopata matatizo ya magonjwa mbali mbali.
Kadhalika aliongezea kuwa atalisimamia vilivyo suala la upatikanaji wa madawa ambayo yanasambazwa na bohari kuu ya Madawa (MSD) kuwa yanawafikia walengwa kwa wakati katika ngazi zote za zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitalini lengo ikiwa ni kuhakikisha kila mwananchi ana pata haki sawa bila ya kufanyiwa ubaguzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.