Picha na maktaba. |
KAHAMA Mtu mmoja aliyekuwa kondakta wa basi la Prince linalofanya safari zake kati ya Shinyanga na Dar es salaam amefariki dunia baada ya kukanyagwa na gari wakati akidandia kwenye basi hilo baada ya kumaliza kupima katika Muzani wa magari Eneo la Tinde wilaya ya Shinyanga vijijini.
Kwa mjibu wa kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amemtaja aliyefariki kuwa ni Masumbuko Kidanga mwenye umri wa miaka 40 na ambapo tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 alfajili ambapo mtu huyo alikanyagwa wakati akidandia basi hilo na kuteleza na akaingia kwenye taili za Nyuma na kufa papo hapo.
Amesema kuwa basi lililomkanyaga lina namba za usajili T 676 AAC mali ya Kampuni ya Princes Anam linalifanya safari zake kati ya mwanza na Dar es salaam ambapo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Salumu Zacharia mkazi wa Mwanza.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekamatwa na anahojiwa na jeshi la polisi ili kupata ukweli wa tukio hilo na kwamba baada ya mahojiano atafikiswa mahakamani kwa kosa la uzembe wakuendesha gari.
WAKATI HUO HUO Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kufanya mauwaji wa kijiji cha Nyankende ambapo walimuuwa mama mmoja Bi. Mwajuma Maige mwenye umri wa miaka 35.
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha mkuu wa upelelezi wilaya ya Kahama Bw. George Bagyemu amewataja washukiwa hao kuwa ni Paschal Lulahuja na Jurdan Lulahuja ambao walitekeleza tukio hilo usiku wa kuamkia jana majira ya saa 8 usiku.
Bagyemu amesema kuwa chanzo cha tukio hilo kuwa ni migogoro ya kimahusiano ambapo watuhumiwa ambapo Bw. Paschal Lulahuja alikuwa ni mkwe wa Mwajuma Maige na alikuwa na tatizo la upofu wa macho na kumhisi kuwa amefanyiwa vitu vya kishirikina.
Hata hivyo Mtuhumiwa Jurdan Lulahuja na mwenzake ambaye anatafutwa na polisi walipatiwa kiasi cha shilingi laki 3 na Pachali Lulahuja ili waweze kwenda kutekeleza mauwaji ya mama mkwe wake ambaye anadaiwa kuwa alikuwa akipa kiburi mke wake ili waachane na baada ya kupatiwa fedha walikwenda kumuuwa kwa kumukata mapanga
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.