ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 27, 2015

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA RORYA NA LAMECK AIRO.

Amekuwa kiongozi wa kwanza kusimikwa uchifu kimila na hii ni ishara ya kukubalika, wananchi wa jimbo la Rorya walipata wakati mgumu kumshawishi tena kurejea na kuwatumikia. Pichani wazee wa kimila toka vijiji na kata mbalimbali za wilaya ya Rolya wakimkabidhi mkuki na ngao mgombea nafasi ya ubunge jimbo hilo kupitia CCM,  Lameck Airo kama ishara ya ulinzi na dhamana ya kuwaongoza tena.
Wahamasishaji wakifurahia yao.
Mwenyekiti wa wilaya ya Rorya Namba 3 (kushoto) ndiye aliyemkabidhi Ilani ya CCM uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Licha ya kuyataja mambo aliyoahidi na hatimaye kuyatekeleza katika kipindi chote kilichopita akiwa katika nafasi ya ubunge ikiwemo kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kisasa kwa akinamama wajawazito, kuboresha vituo vidogo vya afya, ujenzi wa barabara na ukarabati wake kwa kipindi chote akiwa madarakani pamoja na uboreshaji ofisi za ulinzi na usalama  wa jeshi la polisi hasa ikizingatiwa kuwa wilaya hiyo ilikuwa na historia ya kuzuka matukio mengi ya wizi wa mifugo toka kwa watu nchi za jirani, pia mgombea huyo nafasi ya ubunge Jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo, aliainisha vipaumbele vyake katika utekelezaji ilani ya CCM 2015 -2020.
Mratibu wa kampeni za Lameck Airo Bw. Daniel Lameck hapa akisalimia maelfu ya wananchi wa jimbo la Rorya katika mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimboni humo. 
Kwa umakini wananchi wakisikiliza sera.
Ili kupata ridhaa ya wananchi hapa mbunge anayetetea nafasi yake jimbo la Rorya Lameck Airo alipata fursa kuzungumza na wananchi wake na kuakianisha sera za CCM kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.
Toka kwa enzi na enzi vizazi na vizazi CCM nambari wani.
Timu ya ushindi mbio za kampeni CCM wilaya ya Rorya.
Ishara ya kukubalika.
PICHA ZOTE: ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.