ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 27, 2015

MGOMBEA UBUNGE CCM JIMBO LA NYAMAGANA AANIKA VIPAUMBELE VYAKE KWA WANANCHI .


MGOMBEA nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Nyamagana wa Chama Cha Chamapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula, ameweka wazi viapaumbele vyake kwa wananchi wa jimbo hilo ili wamuchague Octoba 25 mwaka huu.

Mabula akihutubia mamia ya wananchi waliofurika  jana kwenye viwanja vya Mbugani wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama hicho Wilaya ya Nyamagana, alivitaja viapaumbele kuwa ni Afya, Elimu, Maji safi, Miundombinu ya barabara za mawe na lami, Umeme, Ardhi,Uchumi.

Akizungumzia Afya alisema kwamba atakapochaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha Kata zote 19 za jimbo hilo zinajenga vituo vya afya ili kusaidia wananchi kupata huduma hiyo badala ya kutegemea Hospitali ya Wilaya iliyopo katani Butimba na Hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Seko-Toure.

Mabula aliwahakikishia wananchi kuwa katika suala la Miundombinu, atasimamia ujenzi wa barabara za mawe katika maeneo ya miinuko na vilimani ili kurahisha usafiri na kujengwa barabara za lami katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya Kata pamoja na kuboresha zilizopo pembezoni kwa kiwango cha chagalawe.

“Ntapigania kuhakikisha mtandao wa maji safi na salama unafika katika maeneo ya makazi ili kupunguza adha kwa wananchi hasa walioko katika vilima na walio pembezoni mwa jiji kwa kuchimba visima virefu wakati tukiendelea kupigania maji safi ya bomba yanayotoka ziwa Victoria kuwafikia,”alisema.

Mabula alisema kuhusu Uchumi atasimamia yaliyopo kwenye Ilani ya CCM ya uwezeshwaji wa mitaji “Fedha” kwa vikundi vya wajasriamali wanawake na vijana wakiwemo wafanyabiashara wadogo (Machinga) ili kuwawezesha kujiinua kiuchumi na kukuza biashara zao pamoja na kuwatengea maeneo ya biashara na kuyaboresha yaliyopo.
  
Mabula pia aliwaomba wananchi wa jimbo hilo wamchague ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ikiwemo upungufu wa walimu na ujenzi wa matundu ya vyoo na madarasa ili kuweka kuboresha mazingira.

“Wananchi nikipata lidha yenu na kuwa mwakilishi wenu sitawangusha kwa kuhakikisha tunafikisha umeme maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, lakini pia suala la ardhi tutahakikisha Hati za umiliki wa ardhi zinatolewa haraka na maeneo yanayopimwa na kuchukuliwa na serikali kwa huduma za kijamii mnalipwa fidia stahiki,”alisema.

Mabula aliwahakkishia vijana kuendeleza sekta ya michezo ili kusaidia kutoa ajira na kuboresha mashindano aliyoyaasisi ya  Meya Cup kwa kuyatanua yaweze kuwa ya Jimbo zima na kuwa na zawadi kwa washindi ambazo zitawezesha kuwa mitaji ya kujikwamua kiuchumi.

Mkutano huo ulizinduliwa na mgeni rasmi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Livingistone Lusinde maarufu Kibajaji na kuhudhuriwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu na viongozi wa Kamati ya Siasa Mkoa na Wilaya za Nyamagana na Ilemela wakiwemo mgombea wa jimbo la Ilemela Angelina Mabula na madiwani kutoka majimbo yote mawili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.