Airtel Imetangaza washindi wa
droo ya nne ya “Jiongeze na Mshiko”
• Washindi wazawadiwa pesa taslim.
·
Zaidi ya milioni 90 bado kushindaniwa
Dar es Salaam, Agosti
11, 2015, Airtel Tanzania imetanga washindi
wa droo yake ya nne ya promosheni
ya "Jiongeze na Mshiko" katika ofisi za makao makuu ya Airtel zilipo
Morocco jijini Dar Es Salaam, ambapo wateja wanaweza kushinda zawadi ya fedha
kila wiki ya shilingi tatu , milioni
moja na mwisho wa promosheni mteja ataweza kuondoka na kitita cha
shilingi milioni 50.
Akiongea wakati wa droo hiyo
,Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki alisema leo tunatangaza washindi wawili wa promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo watajishindia pesa taslim
shilling milioni tatu na milioni moja kila mmoja. Ninayo furaha kutangaza
washindi hao ambao ni Josephat Mahinda(25) Askari Magereza wa wa
Mkoa wa Manyara yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na mshindi wa pili
ni Daudi Ally Kingonji (31) mfanya biashara
na mkazi wa Kiwalani Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1.”
Kaniki aliongeza kwa kusema, mpaka sasa Airtel imeshakabidhi
zawadi kwa washindi mbali mbali hapa nchini. Na leo hii tumewakabidhi washindi
wa droo ya tatu ambao ni Shangai
Rodger (53) mkazi wa Tanga yeye amejishindi shilingi milioni 3 ,
na mshindi wa pili ni Afrillious Kapinaa
(21) mwanafunzi na mkazi wa mkoa wa Dar Es Salaam yeye amejishindi
shilingi milioni 1 waliopokea zawadi zao leo
hii asubuhi.
Akiongea na waandishi wa habari Afrillious Kapinaa mwenye
umri wa miaka 12, aliishukuru Airtel kwa kuanzisha promsheni hii. Ushindi wake
ulikuja kama bahati na msaada mkubwa sana katika maisha yake ya uanafunzi.
“Wazazi wangu wako Songea, ushindi huu wa milioni moja utanisaidia kutimiza
mahitaji yangu nikiwa hapa chuoni.
Nawahimiza Wateja wengine wa Airtel kujiunga na prmosheni hii kwani ya ukweli
kabisa”.
"Tunawashukuru wateja wetu na watanzania wote
walioshiriki mpaka sasa katika promosheni hii. "Tunaamini ushindi huu
utawawezesha wateja wetu kupata fedha za kuendesha shughuli zao za kiuchumi na
kuboresha maisha yao, hilo ndilo lenge letu kama Airtel. Natoa wito kwa
watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma ujumbe wenye neno BURE kwenda
namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia droo zetu za kila wiki."
alimalizia Kaniki.
Tupe maoni yako



0 comments:
Post a Comment