ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 22, 2015

BREAKING NEWS: SUMAYE AJIUNGA NA UKAWA.

CHAMA Cha Mapinduzi, CCM, kimetikiswa tena leo Agosti 22, 2015, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mh. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na UKAWA.

Sumaye ametangaza uamjuzi huo mbele ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jioni hii pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam.

Ni mahala hapo hapo ambapo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa, alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Sumaye anakuwa mtu wa pili wa CCM aliyewahi kushika wadhifa wa juu serikalini kutangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Pichani Sumaye akiwa meza kuu na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, anayewakilisha vyama vya UKAWA, Mh. Edward Lowassa, na viongozi wengine wa UKAWA.

Akieleza sababu za kukihama chama hicho, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi na kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hicho,  waliokuwa wakizunguka nchi nzima, walijielekeza zaidi kjuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura. "sitoki CCM labda nina hasira na ccm, au sikutchaguliwa kwa vile sikuteuliwa, na wala sitoki CCM ili kudhoofisha chama cha Mapinduzi, na badala yake nakiimarisha." alisema wakati akitangaza kujivua uanachama wake.

Kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli, amesema na kjuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakishwa mabadiliko hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.