Kikosi cha timu ya Kilimani Mashariki kilichotowa dozi kwa timu ya Kisimajongoo cha kipigo cha bao 3--0 wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Kikosi cha timu ya Kisimajongoo kilichopata kipigo cha mabao 3--0 na timu ya Kilimani Mashariki
Kocha Abdulhani Msoma akifuatilia michezo ya Bonaza katika uwanja wa mnazi mmoja kushoto Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni na kulia Mchezaji wa Zamani wa timu ya Nyuki. iliokuwa na makazi yake kikwajuni Zanzibar.
Kizazaa katika goli la Kilimani Mashariki hakuna madhara yaliotokea
Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia michezo ya Bonaza ya Kombe la Masauni linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.
Mchezaji wa timu ya Kisimajongoo akimpita mchezaji wa timu ya Kilimani Mashariki.
Kocha wa timu ya Kisimajongoo akitowa maelezo kwa wachezaji wake kuweza kurudisha bao na kuongoza mchezo huwa wakiwa nyuma ya bao moja wakati wa mapumziko.
Mchezaji wa timu ya Kilimani Mashariki akimpita mchezaji wa timu ya Kisimajongoo.
Mchezaji wa timu ya Kisimajongoo akimkata mtama mchezaji wa timu ya Kilimani Mashariki wakati wa mchezo wa Bonaza kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka
Golikipa wa timu ya kisimajongoo akigagaa baada ya mpira kuingia golini ikiwa bao la pili la timu ya Kilimani Mashariki.
Mchezaji wa timu ya Kilimani Mashariki akiifungua timu yake bao la tatu katika mchezo huo wa Kombe la Masauni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar
Mchezaji wa timu ya Kisimajongoo akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Kilimani Mashariki akijiandaa kumzuiya.
Wachezaji wa timu ya Kilimani Mashariki wakishangilia bao lao la tatu na la ushindi wakati wa mchezo wao na timu ya Kisimajongoo mchezo uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja
Wachezaji wa timu ya Kilimani Mashariki wakishangilia ushindi wao baada ya mchezo kumalizika kwa ushindi wa mabao 3--0
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.