ISHA MASHAUZI KUPAKUA KITU CHAKE KIPYA JUMATANO HII …ni
mwendelezo wa ‘project’ yake nje ya taarab.
Baada ya kufanya vema kwa ngoma zake mbili nje ya taarab
“Nimlaumu Nani” na “Nimpe Nani” Isha Mashauzi anashuka na rumba lingine lenye
mchanganyiko wa vionjo vya mutwashi.
Wimbo unakwenda kwa jina la “Usisahau” ukiwa umepakuliwa
katika studio za Soft Records chini ya producer Pitshou Bampadi “Shemeshaa”.
Isha Mashauzi aliurekodi wimbo huo mwanzoni mwa mwaka huu na
kuuweka kwenye hazina ya nyimbo zake kibao zilizokamilika na kuzihifadhi
kibindoni.
Nyimbo nyingine za Isha Mashauzi nje ya taarab ambazo
zimeshakamilika ni “Ado Ado” uliopigwa katika miondoko ya mchiriku na “Mahepe”
ambao upo katika mahadhi ya Afro Pop iliyochanganywa na vionjo vya muziki wa dansi.
“Usisahau” ni utunzi wake Isha mwenyewe ambapo ameuimba
mwenyewe mwanzo mwisho huku sauti za uitikiaji zikipewa ‘tafu’ na mwimbaji wa
zamani wa Malaika Band - Daddy Diperon “Kiongozi wa masauti ya chini” ambaye
kwa sasa anaitumikia Mashujaa Band.
Magitaa ya solo na bass yamepigwa na Pitshou Bampadi
“Shemeshaa” wakati kinanda kimepapaswa na mkali wa keyboard Fred Mazaka kutoka
Mashujaa Band.
Isha Mashauzi amesema kuwa wimbo huo utakuwa hewani Jumatano
ya Julai 8 kupitia vituo mbali mbali vya radio pamoja na mitandao kadhaa ya
kijamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.