ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 9, 2015

MESSI AMWAGA RASMI WINO AZAM FC KUITUMIKIA MIAKA MIWILI.

Messi (kulia) akiwa ameshika jezi ya Azam FC leo
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIKU mbili baada ya kupewa haki ya kuwa mchezaji huru, winga Ramadhan Yahya Singano ‘Messi’ amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Azam FC.
Azam FC imemtambulisha rasmi Messi leo na kutoa picha mbalimbali, akisaini Mkataba, akikabidhiwa jezi na akiwa na mashabiki wa timu hiyo.


Juzi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), liliamua Messi ni huru na sasa anaweza kujiunga na timu yoyote.


Kikao cha Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF kilichofanyika juzi, klisema Simba SC walishindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya Mkataba, hivyo wanapoteza haki za kummiliki mchezaji huyo.

Messi akisaini Mkataba mbele ya Mwanasheria Mkuu wa Azam FC, Shani
  
Chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, Kamati hiyo ilijiridhisha Messi hakuwahi kupewa nyuma ya kuishi na Simba SC jambo ambalo ni kinyume cha Mkataba baina yake na klabu hiyo.


Simba SC iliwakilishwa na Mwenyekiti wake wa Kamati yake ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch wakati Messi alifika na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA), Mussa Kisoky.  


Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo kwamba imeghushi Mkataba wake.
Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika mwakani.


Lakini Simba SC iliendelea kusistiza mchezaji huyo alikuwa ana Mkataba wa miaka mitatu.


Awali, Sekretarieti ya TFF, chini ya Katibu wake, Selestine Mwesigwa ilizikutanisha pande zote mbili, mchezaji na Simba SC na kuamuru waketi chini na kutayarisha Mkataba mpya baada ya kuona huu wa sasa una mushkeli.


Hata hivyo, Messi alikataa na kuamua kulihamishaia suala hilo Kamati ya Sheria ambayo juzi ilimpa ‘ushindi’.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.