KAHAMA
JESHI la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawatafuta watu wawili ambao wamehusika katika matukio mawili tofauti ya mauwaji ambayo yametokea wilayani humo wiki iliyopita ili waweze kufikishwa mahakamani.
Akizungumuza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha mkuu wa upelelezi kituo cha Polisi wilayani Kahama George Bagyemu amesema jeshi linamtafuta Ntaki Mheziwa mkazi wa mtaa wa Ilindi anayedaiwa kumuuwa mke wake Mwajuma Mganda kutokana na ugomvi wa mali.
MSIKILIZE KAMANDA George
Aidha jeshi hilo linamtafuta pia kijana mmoja ambaye hajatambulika mara moja ambaye alimuuwa mwendesha pikipiki wiki iliyopita katika barabara itokayo Kahama kuelekea Kakola halmashauri ya Msalala na kutokomea kusikojulikana akiwa kwenye harakati za kupora pikipiki hiyo.
MSIKILIZE TENA KAMANDA George
Hata hivyo jeshi hilo linaendelea kuwahamasisha waendesha pikipiki ili kuhakikisha kuwa wale ambao wanawabeba abiria nyakati za usiku kuwa makini nao kwani hao ndio wamekuwa wakisababisha mauwaji kwa waendesha pikipiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.