Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Jidawi akizungumza na Madaktari Diaspora kutoka Washington walipofika Afisini kwake kwa kujutambulisha ujio wao Zanzibar walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiwa chini ya uenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),wakiwa Zanzibar wametoa huduma ya kucheki wagonjwa wa Kisukari na Meno na kutoa Elimu ya Afya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar.
Mkuu wa Ujumbe huo,Rais wa Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Daktari wa Meno akuzungumza wakati wa mkutano huo na Katibu Mkuu Wizaya ya Afya Zanzibar walipofika Afisini kwake kujitambulisha.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Saleh Mohammed Jidawi akipokea msaada wa Dawa
za Binaadamu kutoka kwa Daktari Jummy
Amuwo kwa niaba ya Madaktari wa Dispora kutoka Washington wakiwa Zanzibar mualiko wa Jumuiya ya Watanzania Washingto,
akishuhudia Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid, makabidhiano hayo
yamefanyika katika Afisi za Wizara ya Afya Zanzibar
Wakipongezani kwa ushirikiano waliouonesha kwa mapokezi waliopata wakipongezana baada ya hafla hiyo.
Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Wizara ya Afya Zanzibar, baada ya hafla ya kukubidhi msaada wa dawa
Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar nje ya Jengo Wizara ya Afya Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi dawa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Jidawi.
Picha zote na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.Com.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.