Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI
waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini
Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro
Tanzania Music Awards. Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi 13 June 2015.
Akizungumza na mwandishi wetu,
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli amesema jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania. Washindi hawa wataungana na washindi wengine 4 wa Hapa Dar Es Salaam.
Bi. Pamela
amesema washindi hawa walichaguliwa kwanjia ya kuponi baada ya wao kama wanywaji kununua bia ya
Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni.
Washindi hawa wanalipiwa gharama zote za usafiri, Malazi na chakula kwa kipindi cha
siku zote tatu watakazo kuwa hapa jijini.
Bi. Pamela
amesema washindi wanaokuja nikutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Tanga,
Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama, Musomana Dar es Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.