ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 11, 2015

WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA WATEMBELEA MGODI WA ACACIA.

MAELEZO YAJA


















Meneja wa mgodi wa kuzalisha dhahabu wa ACACIA uliopo Bulyanhulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Bi. Michelle Ash akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea mgodi huo mwishoni mwa wiki.
Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulipo:

§  MKOA – Shinyanga
§  WILAYA – Msalala
§  KATA – Bulyanhulu
§  Vijiji jirani na Mgodi (14) – Namba Tisa, Kakola, Busing’we, Igwamanoni, Ilogi, Buyange, Igudija, Bunango, Bugarama, Busindi, Lwabakanga, Busulwangili, Iyenze, Mwasabuka (Vipo kwenye kata za Bugarama, Bulyanhulu and Mwingiro)
§  Idadi ya watu wanaoishi katika kata tatu zilizo jirani na mgodi ni zaidi ya 47,000

Mgodi wa Bulyanhulu umepanga kutumia dola za kimarekani milioni 3.5 kwa mwaka huu 2015.



Baadhi ya miradi mikubwa mwaka huu ni:

1.     Kituo cha afya cha Bugarama awamu ya kwanza (wodi ya wazazi, jengo utawala,jengo la wagonjwa waanje) Mgodi unatumia milioni mia nane (800)kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mradi wa kuipandisha hadhi zahanati katika kijiji cha Bugarama kuwa kituo cha afya cha Bugarama.
2.     Bwawa kubwa la kunyweshea mifugo wilayani Nyang’hwale
3.     Mchakato wa awali wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka mgodini hadi njiapanda ya kuingia kijiji cha Ilogi
4.     Ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya – Nyikoboko na Nyijundu
5.     Kuwezesha vikundi vya wajasiliamali
6.     Nyumba za walimu katika shule ya msingi Bugarama - Mgodi umetumia shilingi milioni 400 kumalizia nyumba 6 za walimu katika shule ya msingi ya bugarama kata ya bugarama halmashauri ya Msalala. Maboma ya nyumba hizo sita yalijengwa kwa nguvu ya wananchi na serikali, kisha mgodi umesaidia kumalizia maboma kwa kuezeka na kuweka miundombinu yote.
7.     Kukarabati madarasa saba na nyumba mbili za walimu shule ya msingi Busindi
8.     Vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Iyenze na vyoo vya umma kijijini.
9.     Kujenga madarasa mawili na vyoo vya wanafunzi na walimu katika shule ya msingi Rwabakanga
10.                        Vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Bunango
11.                        Kuchimba visima nane virefu vya maji na kukarabati visima sita virefu vya maji.
12.                        Kujenga darasa moja, vyoo vya wanafunzi na kukamilisha nyumba ya walimu shule ya msingi Mwasabuka.
13.                        Kumalizia ujenzi wa zahanati ya Kakola
14.                        Kufanya ukarabati na kupeleka umeme shule ya sekondari Bugarama
15.                        Mradi wa CAN EDUCATE wa kusomesha wanafunzi katika shule za sekondari zilizopo jirani na mgodi: Mwaka huu tuna wanafunzi 900 katika shule 9 kila shule ina wanafunzi 100. Mwaka huu tutatumia Tsh 84,550,000 kwa ajili ya kulipa ada, sare na michango kwa wanafunzi 900.

Changamoto:
Mgodi unakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha unafanya biashara yenye faida, mwaka jana mgodi ulipata hasara ya dola za kimarekani milioni 15 lakini mwaka huu bado haujafanikiwa kurejesha hasara hiyo kutokana na bei ya dhahabu kuendelea kuwa ya chini. Mgodi unafanya mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa unatafuta mbinu za kupunguza gharama za uzalishaji, hata hivyo pamoja na hasara iliyopatikana mgodi utaendelea kusaidia jamii zilizo jirani na mgodi.

Mazingira mazuri kwa wafanyakazi wanaofanya kazi chini ya ardhi mgodini

Mgodi unajivunia kwa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wote wanaofanya kazi chini ya ardhi ili warudi nyumbani wakiwa salama na wenye afya nzuri kila siku. Ndiyo maana mmekutana na wafanyakazi wenye miaka zaidi ya kumi wakifanya kazi chini ya ardhi na wenye afya njema kwa kuwa kampuni huhakikisha wanapatiwa vitendea kazi na mavazi ya kujikinga na hatari zote zinazoweza kutokea. Mfanyakazi haruhiswi kufanya kazi isiyo salama. 

Hivyo kwa sasa tuna wafanyakazi 1800 wanaofanya kazi chini na juu ya ardhi na wote hupewa vifaa vya kujikinga na hatari. Pia mgodi umewekeza katika mtambo mkubwa wa hewa kwa ajili ya kusambaza hewa chini ya ardhi. Mgodi umeenda chini kwa kilometa moja nukta mbili(1.2)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.