SHIRIKA la umeme Tanesco limepiga marufuku kwa wananchi kuachana na vitendo vya kuhujumu miundombinu yao kwa kupitisha nyaya za umeme chini ya ardhi kinyume na taratibu kwani kunaweza kusababisha kutokea kwa majanga ya moto pamoja na vifo.
Hayo yamebainishwa na mkaguzi mkuu wa Tanesco kanda ya Dar es Salaam na Pwani Dismas Mbonde wakati wa oparesheni maalumu ya kufanya ukaguzi wa miundombinu ya Tanesco ikiwemo mita katika Wilaya ya Kibaha.
Mbonde amesema kwamba wamebaini kuwepo majanga ya moto ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mbali mbali kutokana na baadhi ya wateja wao kujiunganishia umeme kinymela kitu ambacho amedai ni hatari kwa maisha kwani wanaweza kupoteza maisha.
MSIKILIZE DISMAS
Kwa upande wake mwandisi mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa mita kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mrisho Sangiwa amesema kuwa kutokana zoezi hilo la ukaguzi wamefanikiwa kuwakamata wateja wao wapatao 26 ambao wanahujumu miundombinu pamoja na kuiba umeme kinyume na taratibu.
MSIKILIZE SANGIWA
Naye afisa usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba amesema kwamba kujiunganishia umeme kinyemela kunaweza kusababisha madhara makubwa ya kupoteza maisha kwani wanaweza kunaswa na umeme.
MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY
Shirika la umeme Tanesco limekuwa likijikuta linapata hasara kutokaana na baadhi ya wateja wake kuiba umeme hivyo umeme mwingi kutumika bila ya kulipiwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.