ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 7, 2015

MKANDARASI KIMEO AKWAMISHA KASI YA MAENDELEO UKEREWE.

NA PETER FABIAN, NANSIO.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, kimeitaka Serikali kupitia Wizara ya Maji kumsimamia kwa karibu Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji safi wa Mji wa Nansio unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 10 kutokana na kusuasua na kutekeleza kwa nyenzo duni mradi huo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alipotembelea eneo la mradi katika chanzo hopo mjini humo na kukuta    wafanyakazi Mkandarasi wa Kampuni ya JANDU Plumbers chini ya Kampuni ya ushauri ya COWI wakipasua mawe kwa kutumia kuni jambo ambalo lilionekana kuchelewesha utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo.

Mtaturu akiwahutupia wananchi wa Mji wa Nansio kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vyaa stendi juzi, alisema kwamba naiagiza kwa uongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA) ya jijini Mwanza ambayo ndiyo msimamizi wa mradi huo kuhakikisha inambana kisawasawa Mkandarasi JANDU  Plumbers  kuwa eneo la mradi na vifaa vya kutekeleza kazi hiyo ambayo amepewa kwa mwaka mmoja.

“Nimetembelea na kukuta wafanyakazi wakipasua mawe kwa kuchoma na moto wa kuni hivi kweli huyu Mkandarasi ataweza kwenda na muda wa kutekeleza kazi hii, lakini cha kusikiktisha ni kuwa na siku mbili baada ya kusikia ntafika kuona maendeleo ya ujenzi huo pia hana vifaa vya uhakikaa katika eneo la mradi husika pamoja na
kulipwa malipo ya awali ikiwani maandalizi ya kuanza kazi,”alisema.

Katibu huyo alisema kuwa CCM kupitia serikali yake ilikubali kutekeleza mradi wa maji safi kwa wananchi wa Mji wa Nansio na maeneo mbalimbali ya wilayani humo kwa lengo la kuhakikisha tatizo la upatikanaji huduma unakuwa wa uhakika ili kumaliza kero iliyopo kwa sasa.

Mtaturu alisema kwamba, serikali imsimamie Mkandarasi huyo na ikibaini hana uwezo wa kutekeleza mradi huo na basi imwondoshe na kumpatia mkandarasi mwingine mwenye uwezo ili wananchi wa Ukerewe waondokane na tatizo la maji ambalo linawakabili, pia kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati kama CCM ilivyoelekeza kwenye Ilani yake ya mwaka 2010-2015 na ikiwemo ahadi ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwa wananchi wa Mji wa Nansio.

“Mkuu wa Wilaya, Joseph Mkirikiti, hakikisha MWAUWASA wanafika na kumsimamia mkandarasi huyu na ikiwezekana toeni taarifa Wizarani ili hatua kali za kisheria zichukuliwe kwani ameisha funga mkataba na kinachotakiwa ni kuanza kuutekeleza kwa wakati ikiwemo kujenga eneo la mradi na kuweka vifaa lakini siyo stahilihii inachelewesha na kuumiza wananchi kusubilia huduma na inaonyesha mradi hauendi umesimama,”alisisitiza.

Mtaturu pia aliwataka wananchi kuanza kuwajadili viongozi waliowapa kuwa wawakirishi wao katika ngazi ya Ubunge na Udiwani kutokana na kusinyaa kwa maendeleo katika Jimbo la Ukerewe na katika maeneo ya Kata zilizo na wapinzani hivyo ni vyema wakajipanga kuwachaguwa wawakirishi wa CCM ambao Chama kinathubutu kuwatumikia wananchi katika kuwaletera maendeleo.

“Siasa si ushabiki angalieni hakuna hata siku moja Mbungea amepiga kelele juu ya Mkandarasi huyu kupata kazi ya ujenzi wa mradi wa maji safi kwa shilingi bilioni 10 na anatekeleza kwa nyenzo hafifu akipasua mawe kwa kuni, Halmashauri pia viongozi wa Halmashauri hii hawalioni hili kuwa ni tatizo hakuna wa kusema hivyo ni vyema wakapisha wananchi wafanye uamuzi wa haki na ulio sahihi kwa manufaa yao na maendeleo kwa ujumla,”alisema.

Mtaturu alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha    wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura badala ya kufanya ushabiki wa siasa kama wa timu za mpira na matokeo yake kuweka vyama na wawakirishi wasiyo na sifa na dhamira ya kuwatumikia kwani maendeleo yanayoonekana ikiwemo umeme vijijini, vivuko na miundombinu ya barabara ilifanywa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Balozi Getruda Mongela wakati huo.

Akizungumza na MTANZANIA, Meneja wa MWAUWASA, Mhandisi Athony Sanga alisema kuwa watafatilia suala la ujunzi wa mradi wa maji safi kama alivyopata taarifa kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa, Mtaturu, na kudai kuwa NJANDU  Plumbers  hajafahamu kilichopo kutokana na Mkandarasi kupewa maelekezo na Wizara chini ya wafadhili wa mradi huo.

“Niseme kwamba tutafatilia kwa ukaribu kama wasimamizi na kuishauri vyema Wizara na ikiwezekana kama itaonekana hana uwezo basi wamuondoe na kuzuia malipo kwa lengo la kumpatia mkandarsi mwingine lakini kwa sasa sina mengi ya kusema zaidi ya kuahidi kufatilia na kutoa ushauri,”alisisitiza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.