Hapa uznduzi rasmi wa Finca Microfinance Bank ukifanyika leo jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa Fedha, Thabit Ndirahomba (katikati), akizungumza katika hafla hiyo. |
Watoto waliokuwepo kushuhudia uzinduzi huo. |
Mmoja wa vijana mcheza sarakasi akionesha umahiri wa kucheza na baiskeli katika uzinduzi wa benki hiyo. |
Wadau mbalimbali, wanahabari na wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. |
Onyesho la kucheza na baiskeli likiendelea. |
Mama akiwa kazini 'chezea kazi wewe. |
Meneja Rasilimali Watu (HRM), Mary Magoire, akizungumza katika uzinduzi huo. |
Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Finca Microfinance Benki, Ed Greenwood akiwasalimia watoto waliokuwepo katika hafla hiyo. |
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. |
Makao Makuu ya Benki hiyo iliyopo Magomeni Mwembechai. |
Wafanyakazi wa benki hiyo wakifuatilia kila tukio lililokuwa likiendelea katika uzinduzi huo. |
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki hiyo (kushoto), Olaf Becker (kushoto), akiteta jambo na Meneja Rasilimali Watu (HRM), Mary Magoire. |
Meneja Masoko Nicholas Madugu (katikati), akizungumza katika hafla hiyo. |
Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Finca Microfinance Benki, Ed Greenwood (mbele), akiongoza wafanyakazi. |
Warembo wa benki hiyo waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali. |
..................................................................................................................
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI YA FINCA Microfinance
FINCA Tanzania MFC Limited, maarufu kama FINCA, ambayo imekuwaikifanya kazi kama taasisi ndogo ya fedha kwa miaka 17 nchiniTanzania, sasa imetangazwa kuwa benki kamili na itajulikana kwa jina jipya la FINCA Microfinance Bank.
Uzinduzi huu ulifanyika Jijini Dar es Salaam Julai 8 mwaka huu.
Benki ya FINCA Microfinance ina matawi 26 nchi nzima na inatoa huduma za kibenki kwa wateja zaidi ya 120,000 mijini na vijijini.
Nafasi ake katika soko imekuwa kikiongezeka siku hadi siku, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika hivi karibuni, kwa wasani wateja wanaofungua akaunti mpya za akiba katika benki hiyo wameongezeka kwa asilimia 44.7
ikilinganishwa na mwaka jana. Hii ni dalili njema katika safari ya mafanikio.
Hii inatokana na mafanikio katika utendaji na ukuaji endelevu wa benki hiyo tangu ianze kutoa huduma za akiba kwa wateja wake baada ya kupokea leseni kutoka kwa Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2013 ambapo FINCA iliruhusiwa kupokea amana kutoka kwa wananchi.
“Hii ni hatua kubwa mno huku tukitarajia kukua zaidi na kuwapa wateja wetu huduma ambazo hatukuwa nazo hapo awali, tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii siku hadi siku ili kutimiza malengo haya na hatimaye Benki Kuu sasa imetukabidhi leseni ya kutoa huduma kama benki kamili.
Tunawashukuru wateja wetu wote ambao wamekuwa nasi tangu mwanzo na kutuwezesha kufikia hatua hii,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FINCA.
“FINCA imekuwa ikifanya kazi zake za ukopeshaji kwa watanzania wengi kwa uadilifu mkubwa kwa miaka 17 iliyopita na tuna furaha sasa kutoa huduma kama benki kamili, na hili litatuwezesha kuwapa wateja wetu
wigo wa kutengeneza ajira na pia kuboresha hali ya maisha yao,” alisema.
Alisema matawi waliyo nayo 26 nchi nzima, yatawasaidia kuwafikia wateja na kutoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tunatarajia kufungua matawi mengine na mawakala katika sehemu mbalimbali nchini hivi karibuni ili kukidhi mahitaji ya huduma za kibenki.
Baada ya kuzindua benki hiyo, alisema watazindua kampeni mpya inayojulikana kama ‘Twende Kidijitali’ ambayo italenga kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuendana na mabadiliko ya kidijitali kwa mfano matumizi ya simu za mkononi kufanya shughuli za kibenki kama vile kuhamisha na kweka fedha.
“Tunaishi katika ulimwengu wa kidijitali na benki mbalimbali
zinalazimika kuendana na mabadiliko haya ili kuhakikisha bidhaa zake na huduma zinatolewa kidijitali zaidi. FINCA haitaachwa nyuma katika hili ndio maana tunajiandaa mapema,” alisema.
FINCA ina zaidi ya mawakala 15 nchi nzima ambao wanasaidia kuziba pengo pale ambapo hakuna tawi na mawakala hawa wanatarajiwa kuongezwa
ili kukidhi mahitaji yaliyopo nay a baadaye.
Alisema, “Wateja wetu watarajie huduma bora kabisa kutoka kwa benki mpya kabisa Tanzania kwa sasa kwani ina wafanyakazi wenye weledi wa hali ya juu ambao wana ari ya kuona ndoto za FINCA zitatimia na pia wateja wanaridhika. FINCA itaendelea kuwahudumia wajasiriamali wadogo
na wakubwa mijini na vijijini ili kuhakikisha watatimiza malengo yao.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.