Afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na vijana Bi. Tausi Hassan, akiwashukuru washiriki kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu warsha hiyo. |
Bw. Ramadhani Hangwa afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na Program ya Idadi ya Watu na Maendeleo, akitoa neno kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue semina hiyo. |
OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA YAENDESHA WARSHA KATIKA HOTEL YA GOLD CREST JIJINI MWANZA KWA AJILI KUHAMASISHA NA KUJENGA UWEZO WA KUJUMUISHA MASUALA YA VIJANA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA NA WILAYA
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Na: Thomas Nyindo
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.