ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 17, 2015

CCM YAAGIZA RC, MULONGO, AMSHUGHULIKIE ALIYEKULA FEDHA ZA WANANCHI WA MTAA WA MALULU KATA YA IGOGO

Katibu wa Mkoa wa Chama hicho, Miraji Mtaturu katika moja ya mikutano yake.
 NA PETER FABIAN, MWANZA.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, kimemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, kumchukulia hatua Mwenyetiki wa Mtaa wa Malulu aliyetafuna fedha za wananchi zaidi ya 200 kwa madai ya kupewa namba za nyumba katika Kata ya Igogo wilayani Nyamagana mkoani hapa.

Agizo hilo limetolewa juzi na Katibu wa Mkoa wa Chama hicho, Miraji Mtaturu, wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Igogo wilayani Nyamagana jijini Mwanza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Wilaya ya Nyamagana, kwa lengo la kuhamasishwa wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na juu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye miradi ya maendeleo.

 Pia, Mkuu wa Jeshi la Polisi (RPC) Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu na wanasiasa wanaohamasisha vijana kuchana bendela za CCM kwa kuwa wanafanya makosa kutokana na kila Chama siasa kusajiliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kupata lidhaa ya kufanya siasa kwa kushindana kwa hoja na sera.

Mtaturu, alisema kwamba wananchi wa mtaa wa Malulu zaidi ya 200 walichangiwa fedha na Mwenyekiti wao Yona Mpuya (CUF) lakini akatafuna fedha hizo kwa kushindwa kuziwasilisha Halmashauri ya Jiji la Mwanza Idara ya Ardhi na Mipango Miji ili kuwapata Namba za nyumba wananchi wa mtaa wake.

 “Kupitia mkutano huu naagiza, Mkuu wa Mkoa, Mulongo ashughulike naye huyu mwenyekiti Mpuya hadi atakaporudisha fedha za wananchi alizotafuna ndani ya wiki mbili, lakini pia kunawenyeviti wa baadhi ya mitaa ambao wanatokana na vyama vya upinzani wanaowazuia wananchi wa maeneo yao kuchangia miradi ya maendeleo awachukulie hatua za kisheria,”alisisitiza.

Aidha aliongeza kuwa, Serikali ya Mkoa, Halmashauri na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wameanza kufanya uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kiasi cha zaidi shilingi 208 kwa miaka minne zilivyotumika kinyume na utaratibu wa kisheria katika kuchochea maendeleo katika Kata 12 za Wilaya ya Nyamagana.

 “Wananchi mpewe taarifa za fedha hizo zilivyotolewa na kutumika kufanya shughuli zipi za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuchochea katika Kata za Mirongo, Mbugani, Isamilo, Pamba, Igogo, Mkuyuni, Butimba, Mkolani, Buhongwa, Mahina na Igoma,” ilisisitiza.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mtaturu, alisema kwamba, Halmashauri ya Jiji chini ya Meya wa Jiji hilo, Stansilaus Mabula, tangu Jiji lilipogawanywa na uongozi kuchukuliwa na CCM limetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba 68 vya maabara katika Kata zote 12, sekta za Afya, Elimu, Maji, Umeme na kutoa mikopo kwa vikundi.

 “Wananchi jitokezeni kujiandikisha kwa wingi katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kurejesha Jimbo la Nyamagana kwa chama cha Mapinduzi kutokana na Mbunge wake wa sasa Ezekial Wenje kushindwa kuwaleta maendeleo kama alivyokuwa akijinadi kwenye majukwa, lakini pia kuwatumikia wananchi kwa kuwagawa hawa wa Chama fulani jambo ambalo hamkumtuma,”alisisitiza.

Mtaturu alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuilinda amani ya taifa hili kutokana na baadhi ya wanasiasa kuanza kutumia vibaya madaraka waliyonayo katika vyama vyao vya siasa kutaka kuwagawa watanzania kwa masilahi yao ya kisiasa huku wakitambua kuwa kukosekana kwa amani na utulivu hakuna mtu wala mwanasiasa atakayepata fursa ya kufanya mikutano ya hadara

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.