MAANDAMANO yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa siku ya tatu kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Wanaharakati wanasema takriban watu sita wameuawa katika makabiliano huku polisi wakitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya watu.
Watu wanachoma magurudumu ya magari na kuweka vizuizi huku nao polisi wakirusha vitoa machozi.
Maandamano hayo kwa mara ya kwanza, yamesambaa kwenda nje ya mji mkuu. Polisi wamezuia wanafunzi wa chuo kikuu kwenye mji ulio kati kati mwa nchi wa Gitega waliojaribu kuandamana kwenda mjini.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu 25,000 wamekimbia nchi hiyo ndani ya majuma mawili yaliyopita, wakihofia kuongezeka kwa ghasia kabla ya uchaguzi mkuu unaokuja.
Ni vijana wenye mabango yakiashiria kukataa maamuzi ya rais wa nchi hiyo kutaka kugombea muhula wa tatu. |
Kamata kamata ya askari nchini Burundi. |
Licha ya Polisi kutumia mabomu ya machozi waandamanaji hawakusita kusonga mbele. |
Waandamanaji nchini Burundi wameingia mitaani katika siku ya tatu sasa kwa hasira baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea nafasi hiyo tena kwa muhula wa tatu. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.