Kizazi
cha tano cha teknolojia ya simu za mkononi (5G) kinategemewa kuwa nguzo muhimu
sana ya miundo mbinu katika ulimwengu ujao wa teknolojia. Hayo yamesemwa na Bwana Ken Hu, Makamu mwenyekiti wa Kampuni
ya Huawei ambaye kwa kupokezana yeye ndiyeMkurugenzi Mtendaji kwa sasa.
Akizungumza
katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya
simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki
iliyopita, Mr, Hu alisisitiza kwamba
maono ya kuwa na teknolojia ya 5G yatafanikiwa kupitia ushirikiano wa sekta
mbalimbali, ubunifu makini katika teknolojia na mageuzi katika mikakati ya
kibiashara.
“Msukumo
mkubwa wa kuwa na teknolojia ya 5G unahusisha mahitaji ya kumwezesha mtumiaji
kupata urahisi kutumia, uwezekano wa vifaa vingi zaidi kutumia Internet katika
maisha ya kila siku, na mahitaji ya kuwa na watoa huduma wanaozingatia sekta
maalum pekee katika mapinduzi ya viwanda siku zijazo” Alisema Bwana Hu.
Aliendelea
kusisitiza kwamba, “Mitandao inayotumia teknolojia ya 5G ikitumika ipasavyo
inaweza kufikia zaidi ya vifaa vya kielektroniki bilioni 100 duniani kote.
Uwezo huu ni muhimu sana katika teknolojia”. Bwana Hu alieleza kitaalamu
kwamba, teknolojia ya 5G ina uwezo wa kufanya kazi na kutoa majibu sahihi kwa
haraka sana (One-Millisecond latency), hili litarahisisha utengenezaji wa
magari yanayojiendesha yenyewe, na matumizi ya viwandani ambayo huhitaji
teknolojia inayofanya kazi kwa haraka sana.
Teknolojia
ya 5G inategemewa kuwa na kasi ya juu sana ya kuhamisha data (10 Gbit/s), hii
itafanya kuhamisha sinema ya ukubwa wa 8G HD kuchukua muda mfupi sana. Sinema
ya ukubwa huu inaweza kuhamishwa kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa kutumia
teknolojia ya 3G, au inatumia dakika saba kwa teknolojia ya 4G lakini kwa
kutumia teknolojia ya 5G itatumia sekunde saba tu. “Zaidi ya kuwa imeboreshwa,
teknolojia ya 5G itawezesha uwepo wa miundo tofauti ya biashara na labda hata
uwepo wa viwanda vipya”. Alisema Bwana Hu.
Bwana
Hu aliendelea kusema, ili kufanikisha uwepo wa teknolojia ya 5G watoa huduma
wanapaswa kwanza kushirikiana na kuruhusu mahitaji ya biashara kuleta maendeleo
katika viwango, na ubunifu katika teknolojia. Baada ya hapo sekta hii itahitaji
ubunifu makini sana katika teknolojia, mfano wa ubunifu ni uvumbuzi wa Huawei
hivi karibuni unaoelekea kufanikisha teknolojia ya 5G.
Baada ya miaka mingi ya
utafiti wa kiteknolojia, Huawei imefanikiwa kuendeleza teknolojia ya SCMA na
F-OFDM ambazo zinaruhusu ufanyaji kazi kwa haraka zaidi. Bwana Hu alisisitiza
kwamba sekta ya teknolojia inapaswa kutafiti na kuboresha maeneo mengine pia
hasa usanifu wa mitandao (Network Architecture).
Mwisho kabisa, Bwana Hu
alisema “Tunaamini kwamba mikakati ya namna hii itasaidia watoa huduma za simu
kupata faida zaidi katika teknolojia ya 4G, itachochea uhitaji wa teknolojia ya
5G na pia itafanya waendelee kuwa vinara katika maendeleo ya teknolojia kutoka
4G kwenda 5G.
Kampuni ya Huawei mwishoni
mwa mwezi February ilitangaza rasmi majaribio ya teknolojia ya 4.5G katika
biashara. Ilisema kwamba teknolojia ya 4.5G ambayo itakuwa tayari kwa matumizi
mwaka 2016, itawekakidogo ubunifu ulio katika 5G uwe katika 4G iliyopo sasa.
Eknolojia ya 4.5G itasaidia watoa huduma za simu kuongeza mapato kwa kutoa
huduma ambazo ni bora zaidi kama kuunganisha simu nyingi zaidi, kufanya kazi
kwa haraka zaidi (low latency) n.k huduma ambazo ni bora zaidi kuliko ilivyo
teknolojia ya 4G sasa hivi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.