ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 2, 2015

MKAZI WA KONDOA AKABIDHIWA TOYOTA IST NA WASHINDI SABA WA AIRTEL YATOSHA WATANGAZWA

 Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto) akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
 Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto) akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
Mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 778 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
 Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), akitoa taarifa za ushindi wake kwa ndugu jamaa na marafiki. 
Wafanyakazi wa Airtel wakimsindikiza mmoja wa washindi kucheza muziki kusherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma. 


MKAZI wa Kondoa akabithiwa Toyota IST na Washindi saba wa Airtel yatosha watangazwa • Ashinda gari ya millioni 15 baada ya kushiriki promosheni ya Yatosha Zaidi • washindi 7 wapatikana kupitia droo ya wiki ya 4 iliyoendeshwa siku ya ijumaa.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemkabidhi gari aina ya Toyata IST kwa Bwana Juma Said Alli mkazi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kuiba mshindi katika droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi. 

Zawadi hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 ilikabidhiwa kwa Alli mwishoni mwa wiki na Meneja wa Airtel Kanda ya Kati, Stephen Akyoo. 

 Akizungumza mbele ya vyombo vya habari wakati akikabidhiwa gari hiyo aina ya IST, yenye namba za usajili T778 DCZ, Alli alisema shughuli zake ni ukulima wa mazao mbalimbali katika Kijiji cha Ololimo na ana mke mmoja na watoto wawili. 

“Sikutegemea kushinda ingawa nimekuwa nikijiunga mara kwa mara na kifurushi cha Yatosha, kila ninaponunua vocha za Airtel na ninamshukuru Mungu nimeshinda kutokana na Yatosha ya Shilingi 500 tu. Hivyo nawahimiza watanzania wenzangu wasikate tamaa kwani na wao wanaweza kubahatika kama mimi na kujishindia gari hili zuri,”alieleza Alli. 

 Kwa upande wake Meneja wa kanda ya kati bwana Stephen Akyoo alisema "tunao washindi wengi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Mtwara, Mbeya, Tanga,Mwanza,katavi na sasa Dodoma. 

 Promosheni hii bado inandelea ni rahisi sana kwa kutumia vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au mwenzi moja kwa moja unaunganishwa kwenye droo ya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST kila siku. 

Vifurushi vya Airtel yatosha vinapatikana kwa kupiga *149*99# , au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha au kununua kupitia Airtel Money kwa matumizi yako ya kawaida kabisa unapata nafasi ya kujishindia gari " 

Wakati huo huo Airtel imetangaza washindi saba wa wiki ya nne ya promosheni ya Airtel yatosha waliopatikana kupitia droo iliyofanyika siku ya ijumaa katika makao makuu ya Airtel Moroco, washindi hao ni pamoja na Juma Mapande (30) mkazi wa Pwani, Eusedio Onesmo Kipalile(48) mkazi wa Njombe, Suleiman Daudi Onesmo (20) Mkazi wa Mwanza, Seleman Kikondi Kimu (29) Mkazi wa Morogoro, Hassan Saidi Kimbe(28) Mkazi wa Dar es Saalam, Mohamed Ahmed Hamis (47) mkazi wa Manyara pamoja na Aivan Mbogambi Saigwa (35) Mkazi wa Dodoma Washindi hawa watakabithiwa magari yao wiki hii pindi taratibu zote za makabithiano zikikamilika

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.