ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 25, 2015

KILUVYA UNITED ‘WABISHI WA PWANI’ WAKWEA LIGI DARAJA LA KWANZA


 Na Victor Masangu, Dar es Salaam, Tanzania
 
TIMU ya soka ya Kiluvya united  yenye maskani yake ya kujidai Kiluvya kwa Komba Mkoa wa Pwani imeweza kutawazwa mabingwa wapya wa kivumbi cha ligi daraja la pili (SDL) baada ya kuitandika timu ya Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliolindima kwenye dimba la Karume Jijini Dar es Salaam.
 
Wabishi hao wa Pwani ambao tangu ligi hiyo ya daraja la kwanza walianza kuonyesha dalili mapema ya kuunyakuwa ubingwa huo wa ligi daraja la pili na kuchupa kwa maana ya kupandahadi daraja la kwanza kutokana na juhudi za hali na mali kwa wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi sambamba na mashabiki wamaoneo mbali mbali.
 
Katika mchezo huo wa fainali ulikuwa wa vuta ni kuvute kutokana na atimu zote mbili kutaka kuonyesha nani na mwamba zaidi katika kulisakata kabumbu lakini vijana wa Kiluvy united ndio waliweza kutoka kifua mbele na kusababisha shangwe kubwa kwa washangiliji wa kiluvy united ambao walikwenda kuipasapoti timu hiyo.
 
Kutokanana ushindi huo Kiluvya United sasa inaunganana timu za  nyingine za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa, Katavi FC na Volcano zikishuka daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.
 
Naye mlezi wa timu hiyo Edo almaarufu Master amezungumza na mwandishi wa habari  hizi ambapo amedai lengo lao kubwa ni kufika mbali zaidi hivyo amewaomba wadau wa Mkoa wa Pwani kwa ujumla kuipa sapoti ya kutosha timu hiyo katika kipindi chote cha kivumbi cha ligi daraja la kwanza kitakapoanza rasmi katika siku za usoni.
 
Kwa sasa kila kona ya Tanzania katika medani ya mchezo wa kabumbu wanaizungumzia timu ya Kiluvya united kutoka na kuonyesha umahiri wake katika mashindano mbali mbali ambayo imekuwa ikishiriki hususan katika ligi daraja la pili imeweza kuonyesha soka la kufundishika kupitia kwa kocha wake Yahaya Issa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.