ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 4, 2015

KIGOGO ANASWA NA KUSHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA NOTI NA KUHUSISHWA NA MAUAJI YA ALBINO.

NA PETER FABIAN. MWANZA.
KIGOGO na mwanachama wa Chama kimoja cha siasa mkoani Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi  hapa, akihusishwa na uhalifu wa utengenezaji noti bandia,utekaji na mauaji ya walemavu wa ngozi (albino), katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa.
 
Habari za uhakika zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyetu vya habari vimedai kuwa , kigogo huyo jina linahifadhiwa alikamatwa Wilayani Magu Februari 26, mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku wilayani humo .
 
Kigogo huyo ambaye  anadaiwa, anahusishwa na utekaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mauaji ya watu hao,alikamatwa baada ya kutajwa na washirika wake katika matukio waliyofanya katika sehemu mbalimbali za mikoa ya Kanda ya Ziwa.
 
Habari zaidi zilieleza kuwa kigogo, anahusika kwa karibu na matukio ya hivi karibuni yaliyotokea katika mikoa ya Mwanza na Geita,ambako watoto wawili  Pendo Emmanuel (4) mkazi wa Ndami Kwimba, Mwanza na Yohana Bahati (1) mkazi Ilyamchele, Chato mkoani Geita.

“Mtuhumiwa alikamatwa na makachero wa jeshi la polisi nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa hadi jijini Mwanza anakoshikiliwa hadi sasa.wakati anapekuliwa  nyumbani kwake, alikutwa na noti bandia, ” kilieleza chanzo chetu.
 
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola,alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa kigogo huyo,alisema kwa sasa yuko nje ya ofisi ,hawezi kuthibitisha na kuahidi hadi pale atakapokuwa ofisini leo.
 
“Taarifa hiyo unayoniuliza kwa sasa sina, Sina taarifa hiyo na  siwezi kuizungumzia, kwa sasa niko nje ya ofisini naomba tuwasiliane (kesho ) leo,”alisema  Mlowola.
Hivi karibuni Februari 14 mwaka huu,wakati akiwaapisha wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema watuhumiwa 15 wanaodaiwa kuhusika kumteka na kumsafirisha Pendo Emmanuel hadi hoteli moja jijini hapa, walikuwa wakishikiliwa na polisi.
 
Akieleza alisema watuhumiwa  hao akiwemo baba mzazi wa Pendo, mmiliki wa hoteli hiyo ambayo haikutajwa jina wala jina la mmiliki wake na  wengine waliohusika walikishikiliwa, wengine kadhaa walikuwa wakiendelea kusakwa na polisi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.